Miaka 100 Ya Skauti: Dc Sophia Mjema Aagiza Kuanzishwa Klabu Za Skauti Katika Shule Manispaa Za Ilala
Dc wa Ilala Mhe
Sophia Mjema akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya skauti wilaya ya ilala
uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Kamishna wa Skauti Wilaya
ya Ilala Bw.Crispin Majiya akiongea katika ufunguzi wa kambi ya skauti wilaya
ya ilala uliofanyika katika sekondari ya pugu jijini dar es salaam.
Kamishna Mkuu
Msaidizi Program za vijana Taifa Bw.Omary Mavula akifafanua jambo katika
ufunguzi wa kambi ya skauti wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu
jijini dar es salaam.
Wanafunzi Zahor Habib
(anayesoma) na Riziwani Baruani wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi Dc wa
ilala Mhe Sophia Mjema (hayupo pichani) katika
ufunguzi wa kambi ya skauti wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu
jijini dar es salaam.
Meza kuu, kutoka
kushoto Kamishna wa skauti wilaya ya ilala bw.Crispin Majiya, Mgeni rasmi Dc wa
ilala Mhe Sophia Mjema pembeni yake ni Kamishna Mkuu Msaidizi Program za Vijana
Taifa Bw.Omary Mavula wakisikiliza risala ya wanafunzi katika ufunguzi wa kambi
ya skauti wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Washriki kambi ya
skauti wilaya ya ilala wakiimba wimbo wa taifa wakati ufunguzi wa kambi ya
skauti wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Mgeni rasmi Dc wa Ilala
Mhe Sophia Mjema akizungumza na simu ya upepo mara baada ya ufunguzi kambi ya
skauti wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Mgeni rasmi Dc wa Ilala
Mhe Sophia Mjema ambae ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi ya wilaya akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake na
wanafunzi wanaopata mafunzo maalumu ya scout alipofika kwa ajili ya kufunga
makambi yao ya mafunzo.
Mgeni rasmi Dc wa Ilala
Mhe Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja ya wanafunzi wanaoshiriki
katika kambi ya skauti wakati ufunguzi wa kambi ya skauti wilaya ya ilala
uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Mgeni rasmi Dc wa Ilala Mhe Sophia Mjema akipiga
picha ya pamoja na viongozi wa skauti mara baada ya ufunguzi wa kambi ya skauti
wilaya ya ilala uliofanyika katika sekondari ya Pugu jijini dar es salaam.
Dar
es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza afisa elimu wa
wilaya ya Ilala kuhakikisha kila shule inafanya uandikishaji wa wanafunzi kwa
ajili ya mafunzo ya vikundi vya skauti nakila shule ihakikishe inatoa mwalimu
mmoja kwa ajili ya kusimamia vikundi hivyo.
Mjema ameyasema hayo katika kuadhimisha miaka 100 ya skauti tangu
kuanzishwa kwake 1917 sambambana kuzindua wiki mawasiliano ya anga kwa njia ya
upepo na inteneti kwa skauti ‘Jamboree on the Air (JOTA), Jamboree
on the Internet (JOTI)’ yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar
es Salaam.
“Ikama ya walimu wa skauti ni ndogo natoa agzio kwa afisa elimu kufanya
uandikishaji wa skauti wakike na wakiume katika kila shule na kuhakikisha kila
shule kunakuwa na mwalimu mmoja ambaye atakuwa anawafundisha skauti hao”
Amesema Mhe Mjema
DC Mjema ameeleza kuwa skauti wengi ni vijana wakifundishwa maadili
mema Tanzania itakuwa ni yenye umma bora na watu wake watakuwa na uzalendo na
Taifa la Tanzania.
“Skauti wengi ni Vijana hivyo ni wajibu wao kutengeneza ulimwengu bila
madawa ya kulevya, bila maovu , kutengeneza skauti wazalendo wenye tija na
Taifa la Tanzania, pia wanapopata fursa mbalimbali za nje ya nchi wasisite
kuitangaza Tanzania kwa kueleza mema ya Tanzania ikiwemo Amani, Muungano na
Rasilimali zilizopo” Amesema.
Pia DC Mjema ametoa wito kwa watoto na skauti wote pindi wanapoona
matukio ya kidhalilishaji au kufanyiwa watoe taarifa kwa mamlaka kwa mamlaka
husika kwani serikali ipo kwa ajili yao na itawalinda.
“Wenyeviti wa Serikali za Mtaa, Wakuu wa Wilaya, Mawaziri, mpaka ngazi
ya juu ya Rais chini ya Rais John Pombe Magufuli tutahakikisha tunazilinda na
kuzitetea haki za mtoto hivyo wasiogope kutoa taarifa za unyanyasaji kijinsia
hata kama wakitishiwa maisha yao” Amesema Mhe Mjema.
Katika hatua nyingine DC Mjema amehaidi kushughulikia moja ya
changamoto iliyotolewa na wawakilishi wa uongozi wa skauti kuhusiana na eneo la
kambi na eneo kwa ajili ya kilimo ambapo amewahakikishia uwepo wa maeneo hayo
kwa kumuagiza Mkurugenzi kuwapa kipaumbele pale watakapo ainisha maeneo kwa
ajili ya viwanda vidogo kwani kufanya hivyo ni kuwakwamua kiuchumi.
“Namuagiza Mkurugenzi kushughulikia suala la eneo la kilimo, pia ni
vyema mkaja ofisini kwangu siku ya Alhamisi ili niwakutanishe na Afisa
Maendeleo kwa ajili ya kujadili na kufikia malengo yenye tija kwa skauti na
taifa kwa ujumla” Amesema Mhe Mjema.
No comments