Breaking News

Matembezi Ya Amani Ya Kuadhimisha Kumbukumbu Ya Mauaji Ya Imam Hussein Yafanyika Dar

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya imam hussein, waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuwa wamoja na kuondoa tofauti zao za kimadhehebu.

 Rai hiyo imetolewa jijini dar es salaam na kiongozi mkuu wa waislamu wa dhehebu la shia ithnasheria tanzania shekh hemed jalala wakati wa matembezi ya amani ya kumbukumbu ya mauaji ya mjukuu wa mtume muhammad( s.w.a) ambapo sheikh jalala amesema mauaji ya imam hussein yanatokana na msimamo wake wa kuwatetea waumini wa dini ya kiislamu.

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu  walioshiriki katika matembezi hayo wamewataka waumini wa dini ya kiislamu na na waumini wa dini nyinginezo kuhakikisha wanasimamia msimamo wa iman hussein kwa kupinga dhuruma katika jamii.
Kila ifikapo muharrami 10 ya kila mwaka dhehebu la shia ukumbuka  mauaji ya imam hussein ambae  aliuawa kikatili na mwili wake kukatwa katwa katika jangwa la karbala nchini Iraqi kwa amri ya Yazid bin Muawiyah aliyekuwa mtawala dhalimu wa ulimwengu wa waislam kwa wakati huo.

No comments