Dc Mjema Aingilia Kati Ugomvi wa FFU na Wananchi wa Ukonga Dar
Mkuu
wa wilaya ya Ilala ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mhe.
Sophia Mjema akiongea na wananchi wa eneo la Ukonga Mazizini mapema leo Jijini
Dar es salaam.
Wakazi wa eneo la ukonga mazizini walilojitokeza kumpokea mkuu wa wilaya ya ilala ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mhe. Sophia Mjema kufatia kupigwa na kuporwa mali zao na watu wanaosadikiwa kuwa ni askari wa FFU.
Wakazi
wa Ukonga Mazizini wakishangilia baada ya Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema,
kuwataka wale wote walijeruhiwa kuandika majina yao hili taratibu za kuwapatia matibabu
zianze mara moja sambamba na kuhaidi kuwa wahusika wa tukio hilo wote watachukuliwa
hatua za kisheria.
Dar es Salaam:
MKUU wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni mwenyekiti ya kamati
ya ulinzi na usalama Mhe.Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi cha
FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la Ukonga Dar es
Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo walichofanya
kuwapiga wananchi.
Akizungumza na wananchi alipowatembelea mapema leo na
kujionea hali halisi wananchi wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari
hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana.
Alisema askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu
gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na
kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu
"Kama kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu
ulikuwa uchunguzi ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao
wangetambulika ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa
hiyo nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe
hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua
wananchi" alisema Mhe Mjema.
Aidha Mhe. Mjema ametaka wananchi ambao wameumizwa na
askari hao kwa vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina
ili wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu
utafanyika kuona nini kifanyike
No comments