Hii Ndio Sababu Ya Halima Mdee Kugoma Kujisalimisha Kwa DCI
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaa Halima James Mdee
amesema hajaenda kuripoti kwa DCI kama ilivyotakiwa kwa sababu yeye hajaitwa
rasmi.
Mdee amesema DCI ametoa tangazo la ujumla, lakini yeye binafsi
hajapewa wito wowote, hivyo hawezi kwenda kutokana na taarifa hiyo.
"Mimi nimesikia tangazo la ujumla, wakiniita in personel
Halima njoo nitaenda na hakuna popote kwenye kauli yao iliposema Halima Mdee
njoo, lakini siwezi kwenda kwa 'general statement', amesema Halima Mdee
Juzi Jeshi la Polisi liliwataka watu wote waliopost kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu askari wao aliye nchini Nairobi wakimuhusisha na
kumfuatilia Tundu Lissu nchini Kenya kwenye matibabu na kutakiwa kuripoti
wenyewe kwa DCI, kabla ya kitengo cha sheria za makosa ya mtandaoni
hakijawachukulia hatua zaidi.
No comments