Breaking News

Mahakama Kuu Kutoa Maamuzi Ya Mapingamizi Cuf 25 August 2017.


Mahakama Kuu ya Tanzania Mbele ya Msajili (Registrar of High Court) kwa niaba ya Jaji Mwandambo imetoa maamuzi ya maombi madogo ya kuhifadhi hali ilivyo sasa (Maintenance of Status Quo) kwa kueleza kuwa haioni tishio lolote kwa muda huu mfupi wa siku 9 mpaka Tarehe 25 August, 2017 siku iliyopanga kutoa Maamuzi ya mapingamizi yaliyowekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomwa kwa uhamuzi huo Naibu mkuu wa kitengo cha habari Bw, Maharagande Mbarala alisema mhe Jaji Mwandambo kimsingi amesisitiza kusubiri siku hiyo na mahakama imejizuia kutoa Amri yeyote kwa sasa.

“Mahakama imetoa maamuzi ya maombi madogo ya kuhifadhi hali ilivyo sasa (Maintenance of Status Quo) kwa kueleza kuwa haioni tishio lolote kwa muda huu mfupi wa siku 9 mpaka Tarehe 25 August, 2017” Alisema Maharagande.


Aidha Bw, Maharagande aliongeza kuwa kufatia uhamuzi huo mahakama amewataka wanachama wapenzi wa chama cha wananchi (CUF) kuwa na subira mpaka tarehe 25 siku ambayo mahakama itatoa maamuzi ya pingamizi hilo.

No comments