TCU YABADILI MFUMO WA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MWAKA WA MASOMO 2017 / 2018
Profesa
Eleuther Mwageni.
Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema maombi ya kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka
wa masomo 2017/2018 yatatumwa moja kwa moja vyuoni.
Kaimu
Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni amesema hawatapokea maombi ya
kujiunga na vyuo vikuu kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
Maombi
ya kujiunga na elimu ya juu yataanza kupokelewa rasmi Julai 22 kwenye vyuo
vyote vya elimu ya juu nchini.
“Wanafunzi
wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wasisite kuchagua vyuo wanavyovipenda na
kuhakikisha wanakuwa makini na programu zilizowekwa na vyuo iwapo zinatambuliwa
na Tume,” Amesema.
Amesema
TCU haitatoza ada yoyote ya udahili kwa waombaji.
No comments