KAULI YA ZITTO KABWE KUFATIA ANNA MGHWIRA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA RC KILIMANJARO
Rais
Dk. John Magufuli jana amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna
Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo wa chama cha
upinzani, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck Sadiki.
Baada
ya kukaa kimya kufuatia uteuzi huo hatimayeLeo Jumapili June 4,2017 Kiongozi wa
AICT Wazalendo Zitto Kabwe ametoa ujumbe yafuatayo:
"Nimekuwa
naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka
katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za
masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea
nchini.
Ninawataka
wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu
maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.
Kabwe
Zuberi Ruyagwa Zitto,Mb
Kiongozi
wa Chama"
No comments