DC HAPI AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA BARAZA LA BIASHARA WA WILAYA YA KINONDONI ASISTIZA UMAKINI KATIKA KUKUSANYAJI WA MAPATO
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akifungua
mkutano wa kwanza wa wa baraza la biashara wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
salaam.
Washiriki wa mkutano huo wa baraza la biashara wilaya ya kinondoni kutoka taasisi mbalimbali jijini Dar es saalm.
Washiriki wa mkutano huo wa baraza la biashara wilaya ya kinondoni kutoka taasisi mbalimbali jijini Dar es saalm.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameitisha
mkutano wa kwanza wa baraza la biashara wa wilaya ya Kinondoni ili kujadiliana
na wafanya biashara kuhusu masuala ya biashara.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mhe
Hapi ambaye ni mwenyekiti wa baraza la biashara alisema lengo la kukutana
na wadau hao ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara na mamlaka husika kujadili
changamoto zinazowakabili na kutathmini mwenendo mzima wa biashara.
Alisema kumekuwepo na changamoto kubwa katika
ukasanyaji wa mapato hasa kwa wadaiwa sugu kutotaka kulipa kodi hivyo kuziagiza
mamlaka husika kuimarisha mfumo mzima wa ukusanyaji kodi.
“ili nchi ikue kiuchumi amewaagiza maofisa biashara
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu
wamachinga wote kutambuliwa kwa kupewa vitambulisho na kulipia kisheria hivyo
ni vema kuwekewa utaratibu huo badala ya kujikuta wakitapeliwa hovyo na
matapeli” alisema Mhe Hapi
Aidha amewaomba wananchi kuwafichua watendaji wa
serikali ambao wana tabia za kutoa kauli za vitisho au kukatisha tamaa kwa
wafanyabishara wakati wa kukusanya malipo ya kodi.
Pia mhe Hapi
amewaonya wale wote wanaoghushi leseni za biashara au nyaraka za
serikali kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kuwa
hatua kali zitachukuliwa wakibainika.
No comments