WATUMIAJI WA HUDUMA ZA TRENI ZA ABIRIAWATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Watumiaji wa huduma
za usafiri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa
kuzingatia sheria za matumizi ya usafiri huo ili kuepuka adhabu ya kufungwa
jela miezi sita.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka uongozi wa TRL umeainisha kuwa matumizi ya usafri wa abiria unasimamiwa
na sheria,kanuni ,taratibu na masharti maalum. Mojawapo limetajwa ni
kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.
Uongozi katika
taarifa hiyo umesisitiza kuwa endapo mtu atafanya kosa hilo atafikishwa
mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisiochopungua miezi sita.
Taarifa hii imetolewa
baada ya kuonekana kushamiri vitendo vya kuvunja taratibu za usalama za usafiri
wa treni.
Aina hii ya uvunjaji
huo wa matumizi yasiyo salama mwaka jana Agosti 03, 2016 yalisababisha , mtu
mmoja kupoteza maisha baada ya kugongwa na geti la lango la kuingilia treni
Stesheni.
Marehemu alikuwa akinining’inia nje ya behewa wakati wa treni ya Pugu
majira ya jioni ikiingia ndani ya eneo la kituo kikuu cha Dar es Salaam.
Uongozi wa TRL
umefafanua kuwa tofauti ya usafiri wa basi ni kwa vile kondakta anaweza
kusimamisha basi ili kumshusha mtu anayening’inia nje lakini kwa treni jinsi
ilivyo ndefu hilo haliwezekani kufanyika kirahisi.
.
Aidha katika taarifa
hiyo Uongozi uimetoa wito kwa wasafiri na wananchi kwa jumla kufuata masharti
ya usafiri wa treni za jiji hasa wale wanao tumia treni ya iendayo Pugu.
Ili
kuepuka maafa na pia kuchukuliwa hatua za kisheria ambazo zitasababisha mkosaji
kufungwa jela..
Wakati huo huo Kikosi
cha Polisi Reli kimeanza operesheni ya kuwadhibiti abiria ambao hawataki
kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya usafiri salama wa treni na
hasa kwa kuning’inia nje ya mabehewa wakati treni ikitembea.
Aidha operesheni
hiyo itahusisha kuwafikisha mbele ya sheria wasafri wote watakaokamatwa
wakienda kinyume na masharti ya usalama wa usafiri wa reli.
Imetolewa na Afisi ya
Uhusiano:
Kwa niaba ya Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Shaban Jumbe
Kiko,
Mei 17, 2017
DAR ES SALAAM
No comments