Breaking News

POLISI INAWASHIKILIA WATU 4 KWA KUPASUA MAITI ILIYOKUWA NA DAWA ZA KUEVYA TUMBONI KATIKA HOSPTALI YA MWANANYAMALA DAR

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wa Nne kwa wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya  katika hospitali ya Mwananyamala jijini dar es salaam.

Akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo kamishna wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam Simon Sirro alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufatia kuwepo kwa taarifa kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana hospitali hapo ambaye anadaiwa kufariki akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Red Carpet iliyopo maeneo ya sinza kutokana na kumeza madawa hayo.

Alisema kutoka na kuwepo na taarifa hizo kikosi kinachoshugulika na kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya kilizifanya kazi na siku ya tarehe 29 mwezi 4 mwaka huu walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wane.

Kamishna Sirro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Omary Abdallah Rukola, Mortuary Attendant mkazi wa Pugu kigogo fresh, Athuman Amiry Mgonja, katika mahojiano na watuhumiwa hao Mortuary Attendant alikili kuuchana mwili wa marehemu kasha kuchukua kete 32  za madawa ya kulevya na kumkabidhi Omary Wagile.

Alisema Omary Wagile ambaye ni mfanyabiashara aliziuza kete hizo kwa Ally Mahamud Nyundo mkazi wa Tabata segerea.

Kamishna Sirro aliongeza kuwa mtuhumiwa Ally Nyundo ni miongoni wa watu waliowahi kutajwa kwenye orodha ya washukiwa wa kujihusisha na matumizi ya madawa  kulevya ya Mhe Makonda ambapo alipimwa na kugundulika kutumia madawa hayo.


Watuhumiwa  hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano, uchunguzi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.