ITEL MOBILE TANZANIA YAMTANGAZA MSANII IRENE UWOYA KUWA BALOZI WAKE NCHINI.
Mwakilishi kutoka
Itel Mobile Tanzania Bw Cooper Chen Ikizungumza katika mkutanoa wa
kumtambilisha balozi wa ITEL Mobile Tanzania pamoja na kutambulisha simu ya
ITEL S31.
Bolozi wa ITEL Mobile
Tanzania Irene Uwoya Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa
kampuni hiyo.
Wa kwanza kuanzia
kushoto Bw Aloyce Michael akishaudia uwekaji wa saini makubaliano, wa pili
kutoka kushoto Balozi wa ITEL Mobile Irene Uwoya, Mwakilishi wa ITEL Mobile bw
Cooper Chen na wa kwanza kilia Bi Asha Mzimbili.
Balozi wa ITEL Mobile
Irene Uwoya na Mwakilishi wa ITEL Mobile bw Cooper Chen wakikabidhiana
makubaliano mara baada ya kutiliana saini.
Meneja masoko Wa ITEL
Mobile Tanzania Bw Wolle Fernando akifafanua jambo katika halfa hiyo.
Washiriki na wadau
kutoka sehemu mbalimbali waliohudhulia halfa hiyo wakipiga piga na balozi wa
ITEL Mobile Tanzania Irene uwoya.
Dar es salaam.
Kampuni ya ITEL
Mobile Tanzania leo imezindua simu mpya aina ya ITEL S31 (Selfie In Low Light)
sambamba na mtambulisha balozi wa bidha zake hapa nchini muigizani Irene Uwoya.
Akizungumza mapema
leo jijini dar es salaam katika hafla ya uzinduzi huo pamoja na kumbabulisha
balozi wa bidhaa zake nchini Meneja Masoko wa ITEL Mobile Tanzania Bw Wolle
Fernando Alisema wamekuwa mstali wa mbele katika kuzalisha vifaa bora ambavyo
vitawapatia wateja wao mawasiliano ya kiwango cha juu cha ubora.
Alisema kampuni kwa
kutambua hilo ITEL Mobile Tanzania imeamua kuingia makubaliano na msanii maarufu
wa filamu nchini Irene Uwoya kuwa Balozi kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kupitia
yeye ataweza kuunganisha Itel Mobile na watanzania.
Bw Fernando aliongeza
kuwa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja jamii itafaidika na kupata elimu juu
ya bidhaa zao hususani kupitia Program wanazozifanya za kusaidia makundi mbali
mbali ya kijamii za Charity Event Programs.
Akizungumzia simu ya
ITEL S31 Bw Fernando alisema kampuni ITEL Mobile mara zote imekuwa mstali wa
mbele katika kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zinakidhi
mahitaji ya wateja wao.
Alisema simu ya ITEL
S31 imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ikiwa na uwezo wa kutunza na
kukaa na chaji kwa kipindi kirefu, kioo chenye ukubwa wa 5.5 Hd, kamera yenye
ubora wa kupiga picha katika mwanga hafifu (Selfie yenye Flash) pamoja na Memory
ya ndani ya simu yenye ukubwa wa 16GB.
Kwa upande wake
balozi wa ITEL Mobile Tanzania Irene Uwoya alisema ni faraja kwake kutokana na
kampuni hiyo kutambua mchango wake kwa jamii hivyo anaona fahari kufanya kazi
na kampuni hiyo ukizingaitia ubora wa bidhaa zake inazozizalisha.
“Najisikia faraja
sana kuteuliwa kuwa balozi wa ITEL Mobile Tanzania kutokana na ubora wa bidhaa
zao wanazozalisha kwa kipindi cha miaka 10 tangu kuanza kutoa huduma zao nchini
hivyo natoa wito kwa watanzaania kutumia simu za ITEL Mobile hususani ITEL S31
Hili weweze kufurahia ubora wake” Alisema Uwoya