KAULI YA MEYA WA ARUSHA BAADA YA KUACHIWA NA POLISI.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbsDehpE6pFGM20uxfuhwa0tQDQ4Oj8eU-yj-5bLpxQA0ZaYN_FMRYVkfxkmXt1PrelVG7I1nTeNEF-Efxd5FwxJhbnShOBYAkiogEgSlAeh1GsmFXrtf7v2IbVEZLu_B9_pWead7zfYnA/s640/1.jpg)
Meya
wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za
rambirambi kwa wafiwa badala ya
kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Aidha
amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa
wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa
kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata
ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.
Meya,
Lazaro aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo
majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.
Amesema
fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake
kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya
kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha hizo kwa malengo mengine na
kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa na kupeleka kwenye misiba ambayo
ilitokea kipindi cha nyuma kama rambirambi.
Amesema
wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni
56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.
“Yani
hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si mimi bali
nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa dini wafanye
sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu nakamatwa kwa kosa
gani ,na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo ambazo ni za rambirambi
bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila
Kata,” alisema na kuongeza;
"Mimi
ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa
Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6
zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo
familia zinakuwepo pale shuleni.
"Moja
ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri wa Kanisa
Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya
zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia.
"Maswali
tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa?
nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki,
walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi
wangu"
Naye Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu
na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya
hatafika mbali.
Awali
jana Mei 19, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati akipokea msaada
uliochangwa na wananchi kupitia tovuti ya
wezesha sasa ambapo alipokea msaada wa takriban shilingi milioni 4
alisisitiza kuwa wanasiasa waache kutumia msiba kwa kuingiza siasa kwani hakuna
fedha yoyote ile iliyoliwa na pia wapo katika harakati za kuwatumia fedha
wazazi pamoja na timu ya wataalam wa afya walioongozana na watoto wa Lucky
Vicent ambao ni majeruhi wanaotibiwa nchini Marekani kama fedha za kujikimu na
kiasi kilichobaki hadi sasa ni zaidi ya
Sh, milioni 56 ambazo kunakamati ndogo ya wazazi iliyoteuliwa ambao wataamua
zitumikaje kwaajili ya kumbukumbu za watoto hao.
No comments