WAZIRI UMMY: TUWAJALI NA KUWASAIDIA BADALA YA KUWATENGA NA KUWAKEJELI WANAWAKE WENYE FISTULA
Jamii imetakiwa kuwajali
na kuwasaidia badala ya kuwatenga na kuwakejeli wanawake wenye fistula kwani kwa
kufanya hivyo kuwatawasaidia kujiona kuwa moja sehemu ya jamii.
Akizungumza mapema
leo jijini dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu alisema hipo haja kwa jamii kutambua umuhimu wa kuwajali,
kuwatunza na kuwaonyesha upendo wanawake wenye ugonjwa huo.
Alisema Tanzania ni
moja ya nchi iliyo na wanawake wengi wenye fistula na jamii imekuwa ikiwatenga
jambo ambalo limechangia wengi wao kukosa matibabu na hivyo kuishi na ugonjwa
huo kwa muda mrefu.
Waziri ummy
alisongeza kuwa hili kutokomeza ugonjwa huo inaitajika nguvu za pamoja hususani
kwa jamii kuwasaidia serikali kuhakikisha wagonjwa wa fistula wanafika katika vito
vya afya hili kupatiwa huduma kwa haraka zaidi tofauti na ilivyo sasa.
“Wanawake wawe
wanajitahidi kufika katika vituo vya afya kwa haraka lakini pia jamii iwasaidie
wapate huduma ili wapone, tofauti na ilivyo sasa kutokana na sehemu kubwa ya jamii
bado wanawatenga” alisema waziri Ummy.
Aidha waziri ummy
aliongeza kuwa serikali katika kuhakikisha inatokomeza ugonjwa wa fistula
nchini katika bajeti bajeti ya fedha ya mwaka huu imepanga kuongeza vituo vya
afya 100.
Kwa upande wake Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Dk.
Hashina Begum alisema lengo la UNFPA kwa kushirikiana na serikali pamoja na
wadau wengine wa afya uhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa fistula nchini.
Alisema UNFPA
ikichukua hatua za makusudi katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa fistula
nchini na kutolea mfano mwaka uliopita pekee zaidi ya wanawake 1,356 wenye
ugonjwa huo walisaidiwa kufanyiwa
upasuaji.