VIDEO; KAULI YA KAMANDA SIRRO KUHUSU SAKATA LA MSANII ROMA

Msanii wa hip hop
Roma Mkatoliki alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika
mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu
wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo asubuhi kuhusukutekwa kwa msanii huyo na
wenzake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro
alisema kuwa hawezi kusema ni lini wasanii hao watapatikana kwani ni hadi pale
upelelezi wanaouendesha utakapokamilika.
Sirro alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyekuwa akiuliza kuhusu lini wasanii watapatikana kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa aliyoitoa jana kuwa hadi Jumapili wasanii hao watakuwa wamepatikana.

==>Haya ni mambo
machache aliyoyazungumza
“Matukio ya utekaji
hayajaanza leo, yamekuwepo na tukafanyakazi tukapata majibu. Tukio hili la
kutekwa wasanii ni la kawaida.
“Tukio hili la utekaji ni kama matukio mengine ya uhalifu ambayo tumeyashungulikia, hatuwezi kusema hali mbaya kwa tukio hili.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.
“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu.
“Wanaosema simu ya Roma ilikuwa inapatikana na kuhoji kwanini hatukwenda TCRA, wasitufundishe kazi, wamejuaje hatukwenda TCRA?
“Wengine walalamika wasema leo ni siku ya tatu tumechelewa kutoa majibu walipo, wajue majibu ya polisi kuuawa tulipata baada ya mwezi mmoja.
“Hawa watu hawakuja kuniambia kuwa Kamishna Sirro sasa tunakwenda kuwateka, kwamba ninajua walipo lakini sitaki kuwakamata."

==> Msikilize
hapo chini akiongea
No comments