MADAKTARI WAFANIKIWA KUWEKA KICHWA CHA BINADAMU ALIYE HAI KUPANDIKIZWA KWA MTU ALIYEKUFA
December 2017 inatarajiwa kuwa siku ya
kihistoria kwenye sekta ya afya na tiba duniani ambapo utafanyika upasuaji wa
kupandikiza kichwa kwa mara ya kwanza utakaofanyika mjini London ikihusisha
madaktari 150 na itachukua zaidi ya saa 34.
Kwa mujibu wa Daktari atakayeongoza upasuaji
huo Dr. Sergio Canavero, upasuaji huo utafanyika kwa mara ya kwanza kwa
binadamu ambapo kichwa cha binadamu aliye hai kitapandikizwa kwenye mwili wa
mtu aliyekufa na binadamu huyo kuweza kupata mwili mpya.
Madhumuni ya upasuaji huu ni kusaidia watu
waliopata magonjwa ya kupooza viungo, watu wenye vilema vya miguu na magonjwa
ya uti wa mgongo kupata matumaini mapya ya kuwekewa mwili mwingine. Upasuaji
huu unatajwa kugharimu zaidi ya Dollar millioni 30.
Upasuaji utafanywa kwa mara ya kwanza kwa
mgonjwa Valery Spiridonov kutoka Urusi ambaye kitaondolewa kichwa chake na
kupandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa. Valery Spiridonov amejitolea
kufanyiwa upasuaji huou kwa sababu ana tatizo la uti wa mgongo liliopelekea
mwili wake kupata ugonjwa wa kiharusi.
No comments