RIDHIWANI AANIKA UHUSIANO WA JAKAYA KIKWETE NA LOWASSA. AELEZA ALIYOPIGIWA SIMU NA BABA YAKE BAADA YA KUPIGA PICHA NA LOWASSA
Mbunge
wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu, Dkt. Jakaya
Kikwete ameeleza uhusiano uliopo kati ya baba yake na Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa kuwa bado ni maswahiba.
Ridhiwani
ametoa ufafanuzi huo kutokana na imani iliyojengeka kuwa kuna uhasama kati ya
Dkt. Kikwete na Lowassa ambao awali walikuwa maswahiba wakubwa kabla ya siasa
kuingiza doa kwenye uhusiano huo.
Uhasama huo uliaminika kuwepo na kuongezeka
hasa baada ya Dkt. Kikwete kuongoza kamati ya maadili ya CCM iliyoliondoa jina
la Lowassa katika orodha ya waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais, hali
iliyopelekea mwanasiasa huyo kuhamia Chadema na kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza
wikendi hii na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo baada ya kuenea mitandaoni
picha inayomuonesha akisalimiana na kuteta na Lowassa, Ridhiwani alieleza kuwa
hakuna uhasama kati ya baba yake na mwanasiasa huyo mkongwe kama wengi
wanavyoamini.
Aliongeza
kuwa amewahi kuwashuhudia wakizungumza na kuwasiliana kama kawaida kwa njia ya
simu mara kadhaa.
“Kwanza
hakuna ugomvi kati ya watu hawa wawili. Unajua watu wanashindwa kuelewa kwamba
hakuna urafiki katika masuala ya kazi. Kwa mfano suala lile la kumtafuta rais,
jambo la kutafuta rais sio jambo la Jakaya peke yake,” alisema Ridhiwani.
“Ukweli
wa mambo ni kwamba Bwana Lowassa na bwana Kikwete ni watu wanaosaidiana katika
mambo mengi sana,” aliongeza.
Katika
hatua nyingine, Ridhiwani alieleza kuwa baba yake alipoona picha yake na Lowassa
wakisalimiana baada ya kukutana Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa kwenye mechi
ya watani wa jadi, Simba na Yanga alimpigia simu kutoka Ethiopia na kumtaka
kuendelea na hali hiyo kwani siasa sio vita.
“Kwa
mfano hata jana jioni alinipigia simu, of course alikuwa yuko Ethiopia,
akaniambia ‘bwana nimeona kwenye picha uko na bwana Edward [Lowassa] ilikuwa
wapi hapo?’, nikamwambia nimekutana nae uwanja wa Taifa tulikuwa tunaangalia
mpira,” “[Akasema] ‘aah naye alikuja kuangalia mpira’ nikasema ndio. Akasema
‘okay hayo ndio mambo mnayotakiwa kufanya, msifike sehemu mkaona kama siasa ni
vita’.
“Kwahiyo
ndio maana mimi baada ya kuongea naye akaniambia siasa sio vita, na mimi
niliposhika simu yangu Instagram yangu nikaandika kwamba ‘tunaendelea
kujifunza…. Lakini basically najifunza kutoka kwa maneno ya mzee wangu ambaye
ameniambia kwamba ‘siasa sio vita na kwamba na ninyi katika umri wenu inabidi
muendelee kujifunza’ kwahiyo hata mimi comment yangu kwenye Instagram, actually
sababu yake kubwa ni hiyo,” alifafanua.
Ridhiwani
alieleza kuwa alimuona Lowassa baada ya kipindi kirefu kupita hivyo aliamua
kumfuata na kumsalimia ambapo pamoja na mambo mengine, Lowassa alimuuliza alipo
Dkt. Kikwete na akampa salamu zake amfikishie na familia kwa ujumla.
Lowassa
alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008 katika Serikali ya
Awamu ya Nne iliyokuwa inaongozwa na Dkt. Kikwete kutokana na sakata la
Richmond.
No comments