KAULI NZITO YA ZITTO KABWE, SAKATA LA GODBLESS LEMA, ATAKA OFISI YA DPP IWAJIBISHWE
Kitendo
cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo
kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe
kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
iwajibishwe
Katika
mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi
kunyimwa dhamana ni siasa za ukomoaji
ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.
"Haitoshi
majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha
mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria
tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya
wananchi" Ameandika Zitto Kabwe
Hata
hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema jana baada ya majaji watatu
kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali
na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na
kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu
kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya
dhamana.
"Mnatufanya
wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka
mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria,
lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia
Lema hadi leo na imetushtua sana". Alisema Jaji Stella Mugasha.
|
No comments