Breaking News

MEYA WA JIJI MH. ISAYA MWITA AIPONGEZA HOSPTALI YA AGHA KHAN KWA JITIHADA ZAKE KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA

Mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa hospitali ya Agha Khan Katika hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kutibu magonjwa ya kinywa na meno jijini dar es salaam
Mwonekano wa Jengo hilo jipya la kisasa la kutoa huduma za matibabu ya magonjwa ya kinywa na meno lilopo katika hospitali ya Agha Khani jijini Dar es salaam
Washiriki wa uzinduzi hafla ya uzinduzi wa jengo hilo wakifatilia tukio hilo la uzinduzi kwa umakini.



Mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akisikiliza maelezo mara baada ya kuzindua jengo hilo la kisasa kutoka kwa wahudumu. 

Na Frank wandiba
Meya wa jiji la Dar es salaam mh. Isaya Mwita amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa ambalo limejengwa katika  hospitali ya Aga khan jijini Dar es salaam ambalo litatumika katika kutoa huduma kutoa ya afya ya kimya kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na meno.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo mapema leo jiji dar es salaam mhe Mwita alitoa pongezi kwa uongozi wa hospitali ya Aga khan kwa kwa juhudi zao za kushirikiana na  serikali katika katika kutatua changamoto mbalinbali zinazowakabili wananchi sambamba na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora hususani katika sekta ya afya.

Alisema serikali ya mkoa inatambua mchango wao kwa jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo pia elimu hivyo kuomba uongozi wa hosptali hiyo kuangalia namna watakavyoweza kupanua wingo zaidi kwa kujenga chuo kikubwa zaidi ambacho kitasaidia jamii pamoja na kuzalisha wataalam ambao watakuwa msaada kwa taifa.

Aidha mstahiki meya mhe Mwita amewataka wafanyakazi wazawa ambao ni waajiliwa katika taasisi hiyo ya agha khan katika Nyanja mbalimbali kufanya kazi zao kwa uadilifu zaidi hili kuweza kufikia malengo ya taasisi hiyo katika kutoa huduma bora za afya na elimu nchini inafanikiwa.  

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi wa tiba ya huduma za meno Dk Mustapha Bapumba alisema kukamilika kwa jingo hilo ni moja ya juhudi za hospitali hiyo katika kuakikisha inatoa huduma bora na kwa ufanisi kwa wananchi.
Alisema kwa kutambua hilo hospitali hiyo waliona ipo haja ya kuwa na jengo linalojitegemea ambalo litatoa huduma ya magonjwa ya kinywa na meno kwa ufanisi zaidi kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi hili kuendelea kuwa msaada kwa jamii nchini.

No comments