KUTOKA MKOANI RUKWA;WATANO KIZIMBANI KWA KUUA KWA MAPANGA NA MASHOKA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA
POLISI
mkoani Rukwa inawashikilia watu watano wakituhumiwa kuwaua kikatili watu watatu
wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Mfinga kilichopo katika Bonde la
Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga kwa kwa kucharangwa na mapanga na mashoka kwa
kile kilichoelezwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwataja marehemu hao kuwa ni
Joachim Kayanda (60), mkewe Evelina Mwanakatwe (47) na mtoto wao wa kiume
aitwaye Emanuel Kayanda (27) .
Kwa
mujibu wa Kamanda Kyando, watuhumiwa hao ambao hakuwa tayari kutaja majina yao
kwa hofu ya kuvuruga upelelezi wa kipolisi unaoendelea, wanaendelea kuhojiwa na
polisi ambapo watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali wa shauri lao
kukamilika .
Alisema
mauaji hayo yalitokea Februari 22, mwaka huu usiku wa manane katika kijiji cha
Mfinga kilichopo katika Tarafa ya Mtowisa iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa
wilayani Sumbawanga.
Akisimulia
mkasa huo, Kamanda Kyando alisema kuwa usiku huo wa tukio watu wasiofahamika
wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, mashoka na marungu walifunga mlango
wa nyumba walimolala wanafamilia hao na kuwaua kikatili kwa kuwakata kata kwa
mapanga na mashoka.
Alidai
kuwa watu hao walifanikiwa kutoroka katoka eneo hilo la tukio muda mfupi baada
ya kutenda unyama huo.
“Chanzo
cha mauaji hayo ni imani za kishirikina kwani familia hiyo ilikuwa inatuhumiwa
kuwa ni washirikina,” alisisitiza.
Na Peti Siyame-Habarileo
Sumbawanga
No comments