DUNIA INA MAMBO! CHEKI PICHA MTOTO AOTA MIZIZI KAMA MTI USONI
Mtoto Sahana Khatum kutoka nchini Dakar ameota mizizi usoni.
Wakati vitu visivyokuwa vya kawaida vilipomea kwenye uso wa
Sahana Khatum, mwenye umri wa miaka 10 miezi minne iliyopita, babake hakushikwa
na wasi wasi.
Lakini wakati vitu hivyo vilianza kusambaa, alishikwa na
wasi wasi na kumlazimu kutoka kijijini mwake na kuelekea mji mkuu wa Bangladesh
Dakar, kutafuta matibabu.
Madaktari sasa wanahofu kuwa Sahana huenda akawa mtoto wa
kike wa kwanza kukumbwa na tatizo linalojulikana kama "tree man
syndrome".
Ikiwa uchunguzi utabainisha hivyo, atakuwa mmoja wa watu
wachache duniani walio katika hali hiyo.
Ni hali ya kijenetiki isiyokuwa ya kawaida ambapo mti humea
hususan kwenye mikono na miguu.
Ni watu wachache ambao wote ni wanaume wanaoaminiwa kuwa na
ugonjwa huo.
Mikono yote ya Abul Bajandar ilimezwa na miti iliyomea yenye
uzito hadi kufikia kilo tano
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa raia
wa kwanza wa Bangaladesh kupatikana na ugonjwa huo, kwa saa amefanyiwa upasuaji
mara 16 na anaweza kuitumia mikono yake.
Madaktari wale wale waliomfanyia upasuaji Abul Bajandar,
tena wanaendesha uchunguzi kubaini ikiwa Sahana anaugua ugonjwa sawa na huo.
Babake Sahana Mohammad Shahjahan ana matumaini kuwa
madaktari watamtibu mtoto wao.
Chanzo-BBC
|
No comments