Breaking News

BUNGE LASIMAMA KUFATIA PAA LA JENGO LA BUNGE KUNG'OLEWA NA UPEPO


Shughuli za ukarabati zinaendelea kwenye jengo ya bunge nchini Ghana baada ya upepo mkali kung'oa sehemu za paa la jengo hilo siku ya Jumanne jioni wiki hii.
Kisa hicho kilisababisha kusitishwa vikao kwa ghafla wakati mvua ilipoanza kunyesha ndani ya jengo kutokana na paa hilo kung'olewa na upepo.

Wafanyakazi walijaribu kukinga baadhi ya maeneo yaliyoachwa wazi kwa kukusanya maji wakitumia ndoo
Jengo hilo lililo kwenye mji mkuu Accra lilikarabatiwa miaka miwili iliyopita.

No comments