BREAKING NEWS: KUTOKA PEMBA MHE MOHAMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA CUF
THE
CIVIC UNITED FRONT (CUF –Chama Cha Wananchi)
TAARIFA
KWA UMMA
Leo
tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani wilaya ya
Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mohamed Habibu
Mnyaa kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12 (6)(7)(16) kutokana na
kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji
dhidi ya viongozi na Chama, kufanya vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha
Chama, kudharau na kushindwa kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila
alipotakiwa kufanya hivyo. Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe
halali 112 kati ya wajumbe wote halali 113.
Wajumbe wote 112 wamepiga kura za
ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba
yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu
wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;
“Kumchukulia
hatua za nidhamu mwanachama au kiongozi yeyote wa tawi hilo, ikiwa ni pamoja na
kumpa onyo, karipio, karipio kali, kumsimamisha uanachama au uongozi wa Chama
kwa muda, na hata kumuachisha au kumfukuza uanachama wa Chama”Mohamed
Habibu Mnyaa alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba mwaka 1999 na
kukabidhiwa kadi yenye Namba ya usajili 029033.
Mohamed ambaye amewahi kuwa
Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni kwa muda wa vipindi viwili 2005-2015, amekuwa na
mwenendo huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake tangu alipokosa ridhaa
ya wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama kumpitisha kugombea kwa mara
nyingine tena katika nafasi ya ubunge mwezi August, mwaka 2015. Mohamed
amefukuzwa uachachama akiwa ni mwanachama wa kawaida wa tawi la Chanjaani
asiyekuwa na wadhifa wowote mwingine ndani ya Chama.
Kwa
mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 108(5) kuhusu Nidhamu ya chama na Muda wa
kukata Rufaa inaeleza kuwa;
“
Mwanachama au kiongozi yeyote aliyeamua kukata Rufaa kwa jambo lolote lile,
basi atafanya hivyo kwa ngazi iliyo juu ya kikao kilichotoa maamuzi ambayo
hakuridhika nayo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne (14) tokea siku
uliotolewa uamuzi huo” ni hiyari yake kuona kama inafaa kukitumia kifungu hiki
au kutokitumia.
Tunatoa
wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani, kuzingatia wajibu wao wa kikatiba
na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda nidhamu na heshima ya Chama chetu
ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla. Uongozi wa tawi hautasita
kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa mwanachama yeyote kwenda
kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama.
HAKI SAWA KWA WOTE
KOMBO MOHAMED MAALIM
KATIBU WA TAWI LA CHANJAANI, JIMBO LA MKOANI-PEMBA
Mawasiliano: 077 815 3414
No comments