TCRA YATISHIA KUZIFUTIA LESENI KAMPUNI ZA SIMU AMBAZO AZIJASAJILIWA DSE
Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetishia kusitisha kwa muda au kufuta kabisa
leseni ya biashara kwa kampuni zote za mawasiliano nchini, zitakazoshindwa
kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
Hatua
hiyo ni kulingana na sheria mpya ya fedha ambayo imetoa ukomo wa hadi Desemba
31 mwaka jana kampuni hizo ziwe zimejisajili katika soko hilo.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam; Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi
James Kilaba amesema kwa sasa wanasubiri maelezo kutoka Mamlaka ya Masoko ya
Mitaji na Dhamana (CMSA) kuhusu idadi ya
kampuni za mawasiliano zilizokidhi sifa za kusajiliwa katika soko la hisa kwa
ajili ya kuchukua hatua kwa zile zilizokaidi kutekeleza agizo hilo la kisheria.
Mhandisi
Kilaba amesema TCRA imeikabidhi CMSA orodha ya kampuni zaidi ya 80 za
mawasiliano, orodha ambayo CMSA itaipitia kwa lengo la kuchuja na kupata
kampuni ambazo zinastahili kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Kauli
ya Mhandisi Kilaba imekuja huku taarifa kutoka soko la Hisa la Dar es Salaam
zikionesha kuwa ni kampuni tatu pekee ndizo zimejisajili katika soko hilo,
licha ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo wake Jumamosi ya Desemba 31 mwaka
ja
No comments