MAREKANI KUMSAKA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN ALIYEAPA KULIPA KISASI
Marekani
imesema kuwa imemuorodhesha mtoto wa
mwisho wa Osama Bin Laden, Hamza, katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa
hilo.
Wizara
ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Hamza Bin Laden ameanza kushiriki
katika maswala ya kundi la al Qaeda, kundi la jihad lililofadhiliwa na babake.
Hamza
amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi maalum
cha Marekani kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wamarekani.
Hamza
amepigwa marufuku kufanya biashara na
raia wa Marekani huku mali zake zikizuiliwa pia.
Mamake
Hamza ni Khairiah Sabar, mmoja wa wake za Osama aliyekamatwa wakati wa
shambulio la wanajeshi wa Marekani kwenye maficho ya Osama mjini Abbotabad
nchini Pakistan mwaka 2011.
Mkuu
wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia ameongezwa
katika orodha hiyo .
Marekani
imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata al-Banna.
Hamza
bin Laden alitambuliwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Qaeda mwaka 2015 na baadaye
akaapa kulipiza kisasi mauaji ya babake mwezi Julai mwaka uliopita.
Katika
ujumbe wa sauti wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama," (Sote
ni Osama), na uliochapishwa katika mitandao, aliapa lazima angelipiza kisasi
mauaji ya babake mwaka 2011 nchini Pakistan.
''Tutaendelea
kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mmejificha ati nyuma ya pazia za
usalama kwa maovu mnayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen,
Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia,'' shirika la habari la
Reuters lilimnukuu.
''Na
kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osama ole wenu,
kwanini sisi tutakuwa tukilinda dini ya kiislamu'' alisema Hamza.
Hamza,
kulingana na wachanganuzi, alitambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi la
al-Qaeda Ayman al-Zawahiri katika ujumbe huo uliolenga kuwavutia vijana ambao
kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.
Hamza
sasa anaungana na nduguye wa kambo, Saad, kuwa miongoni mwa watu wa jamii ya
Osama walioorodheshwa kuwa magaidi.
Chanzo:
BBC
No comments