MAGAIDI WA ISIS WAISHAMBULIA ISRAEL.......WANNE WAUAWA
Kundi la kigaidi linalojiita
‘Islamic State of Iraq and Syria’ (ISIS) kwa mara ya kwanza limetajwa kufanya
mashambulizi ya mlengo wa kigaidi Jerusalem nchini Israel.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin
Netanyahu amesema kuwa shambulizi la kutumia roli lililowaua watu wanne na
kujeruhi wengine 17 lilifanywa na kijana wa Palestina aliyetumwa na kundi la
ISIS.
Israel ilifanya kikao cha
dharura cha kabineti ya usalama ambacho ingawa hakikutoa vielelezo kuhusu mtu
huyo, kilimtaja kuwa mfuasi wa ISIS.
“Tunajua kumekuwa na mlolongo
wa mashambulizi ya kigaidi. Kuna uhakika kuwa kunaweza kuwa na muungano kati
yao [ISIS], kutoka Ufaransa hadi Berlin, na sasa Jerusalem,” alisema Netanyahu.
Mshambuliaji huyo
aliyetambulika kwa jina la Fadi Qunbar mwenye umri wa miaka 28, raia wa
Palestina alitumia lori kubwa kuwagonga watu hao lakini alipigwa risasi na
kuuawa papohapo baada ya kutekeleza tukio hilo.
Watu kadhaa wamekamatwa
kutokana na tukio hilo wakiwemo majirani zake na wana familia wake watano.
No comments