ASKOFU MKUU KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA AMTUMBUA ASKOFU MOKIWA
Mashitaka 10 yaliyofunguliwa na walei 32 wa Kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa,
yamesababisha Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk Jacob Chimeledya
kumvua uaskofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam Dk Valentine Mokiwa.
Hata
hivyo Dk Mokiwa amegomea uamuzi huo kwa maelezo kuwa mwajiri wake ni Sinodi ya
Dar es Saalam ambayo ndiyo yenye uamuzi wa kumfuta kazi na sio askofu mkuu au
askofu mwingine yeyote wa kanisa la Anglikana Tanzania.
Uamuzi
wa kumvua uskofu ulichukuliwa juzi na Askofu Chimeledya baada ya Askofu Mokiwa
kugoma kujiuzulu kama ilivyoshauriwa na nyumba ya maaskofu ambayo ilimkuta na
hatia ya kufuja mali za kanisa hilo na kukiuka maadili ya kichungaji ambayo
yalibainishwa kwenye ripoti ya uchunguzi iliyoundwa na kiongozi mkuu wa kanisa
hilo nchini.
Habari
zilizopatikana kutoka ndani ya kanisa hilo zilieleza kuwa katika kikao
kilichofanyika juzi kanisani Ilala, askofu Chimeledya na ujumbe wake
walihudhuria kikao cha halmashauri ya kudumu ya dayosisi ya Dar es Salaam
akatangaza uamuzi wa kumvua uaskofu Dk Mokiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Licha
ya uamuzi wa kumvua uaskofu, Dk Chimeledya pia aliagiza waraka unaoagiza askofu
huyo kuondolewa madarakani, usambazwe kwenye makanisa yote yaliyoko chini ya
dayosisi ya Dar es Salaam na usomwe jana kwenye ibada mbele ya waumini.
“Ni
kweli kikao hicho kilifanyika jana, Dk Chimeledya alikuja na katibu mkuu na
msajili wa kanisa kwenye kikao, lakini tulishangaa kwamba walikuja na askari
polisi kinyume na utaratibu wa kanisa, alisoma maamuzi hayo aliyodai yametolewa
na nyumba ya maaskofu,”alisema msemaji wa Dayosisi ya Dar es Salaam Yohana
Sanga.
Dk
Mokiwa agoma kung’oka
Katibu
Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam Padri Jonathan Senyagwa jana alisema habari
hizo sio za kweli na barua ambazo zimesomwa katika baadhi ya makanisa jijini
Dar es Salaam zilisomwa kwa makosa.
“Mwenye
mamlaka ya kumfukuza kazi ni yule aliyemwajiri, na mwajiri wa Dk Mokiwa ni
Sinodi ya Dar es Salaam...tutatoa tamko hivi karibuni kuthibitisha kwamba
askofu wa jimbo bado hajafukuzwa,” alisema Padri Senyagwa.
Alisema
waraka ambao umesambazwa na askofu mkuu wa Tanzania haujapitia kwenye
halmashauri ya kudumu ya dayosisi ili kupata baraka zake na wala hauna baraka
kutoka kwa sinodi ya dayosisi jambo ambalo linaufanya waraka huo ukose sifa za
kutekelezeka.
“Ninachokwambia
ni kwamba askofu wa dayosisi ya Dar es Salaam bado ni Mokiwa, hatuzitambui
barua zilizosomwa katika baadhi ya makanisa,” alisisitiza katibu mkuu huyo wa
Dayosisi.
Mgomo
huo pia ulithibitishwa na Sanga, ambaye alifafanua kuwa juzi kulifanyika kikao
kati ya viongozi wakuu wa kanisa na halmashauri ya kudumu ya dayosisi ya Dar es
Salaam na kuelezwa na askofu mkuu wa Tanzania Dk Chimeledya hatua ya kumvua
uaskofu Dk Mokiwa jambo ambalo halmashauri iligoma.
“Tulifanyia
kikao chetu pale kanisa la Ilala, viongozi wetu wakuu walikuja na polisi
wakatusomea huo waraka na kutangaza maamuzi hayo mbele ya halmashauri, lakini
maamuzi hayo yaligomewa na wajumbe wa halmashauri ya Dayosisi ya Dar es
Salaam,” alisema Sanga.
Alisema
halmashauri iligoma kubariki uamuzi huo kwa sababu kanisa la Anglikana Tanzania
lina kanuni na taratibu zake.
Alifafanua
kuwa waraka wa kumwondoa madarakani Dk Mokiwa lazima upate baraka za halmashauri
ya kudumu ya dayosisi na sinodi ya dayosisi.
“Ule
waraka tuliupitia na kubaini kuwa hauna baraza za nyumba ya maakofu, wala hauna
baraka za halmashauri ya kudumu na Sinodi ya dayosisi ndio maana
tuliwakatalia,” alisema Sanga na kuongeza kuwa maamuzi ya kumvua uaskofu Dk
Mokiwa yamefanywa na askofu mkuu wa Tanzania, katibu mkuu na msajili wa kanisa
na sio vikao vya kanisa.
“Ninachosisitiza
hapa ni kwamba askofu wa dayosisi ya Dar es Salaam bado ni Dk Mokiwa, huo
waraka uliotangazwa ni ushawishi wa watu wachache wanaotaka kumchafua kiongozi
wetu wa Dayosisi,” alisema.
Aombwa
ajiuzulu uaskofu
Awali
tume hiyo iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yake, baada ya kubaini makosa
mengi yaliyofanywa na askofu huyo ilimshauri ajiuzulu wadhifa wake na awe
tayari kufanya huduma nyingine ya kumtumikia Mungu.
“Hatua
tunayoichukua ni kwa nia njema kabisa ya kulinusu kanisa letu ambalo limekuwa
naheshima kubwa hapa nchini na duniani kote,”unasema waraka uliosaniwa na Dk
Chimeledya.
Tume
hiyo ilichukua uamuzi huo katika kutatua mgogoro uliopo ndani ya dayosisi ya
Dar es Salaam:
“Nia
yetu ni njema kabisa na hatuna chuki, uhasama wala upendeleo katika jambo hili,
ifahamike kuwa vyombo vyote ndani ya kanisa ikiwemo nyumba ya maaskofu
vinalifahamu jambo hili vyema, hivyo tulitarajia tutaungwa mkono ili kuisaidia
dayosisi yetu ya Dar es Salaam kwenda mbele.”
Pia
waraka huo unaeleza kuwa hiyo sio mara ya kwanza kanisa hilo kufanya maamuzi ya
namna hiyo na kutoa mfano kuwa hata enzi za askofu Mokiwa akiwa askofu mkuu wa
Tanzania alichukua hatua za kulinusuru kanisa lisipotee katika migogoro
mbalimbali ikiwemo mgogoro wa dayosisi ya Tanga ambako alimtaka askofu wa
dayosisi hiyo ajiuzulu kwa hiyari na alikubali.
Baada
ya kutenguliwa uaskofu wa Mokiwa, Dayosisi ya Dar es Salaam itakuwa chini ya
uangalizi wa uongozi wa askofu mkuu mpaka taratibu nyingine za kikanuni
zitakapokamilika.
“Nina
wasii Wakristo wote kwa nieaba ya Bwana Yesu Kristo tuendelee kuwa watulivu
katika kuijenga dayosisi yetu na kanisa la Mungu kwa ujumla.”
Mashitaka
10 ya Mokiwa
Askofu
Mokiwa Machi 2015 alifunguliwa mashitaka 10 ambayo ni kuizuia dayosisi ya Dar
es Salaam kupeleka michango pasipo maelekezo ya sinodi ya Dayosisi ya Dar es
Salaam, kuhamasisha dayosisi kujitoa katika udhamini wa kanisa Anglikana
Tanzania (KAT) kwa lengo la kuifarakanisha dayosisi na jimbo kinyume na katiba
ya dayosisi.
Mashitaka
mengine ni kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria
vya rushwa katika eneo la kanisa la mtoni Buza na miradi mingine, kushindwa
kutatua migogoro inayohusu uwekezaji na maadili baina ya dayosisi na mitaa ya
Magomeni ambao kuna mgogoro na Benki ya DCB, kanisa la Kurasini na mengine.
Askofu
huyo pia anadaiwa kushindwa kutatua migogoro baina ya mapadiri na waumini na
kutunza mali za kanisa katika mtaa wa Watakatifu wote Temeke na kutelekeza
nyumba ya askofu iliyopo Oysterbay ambako imegeuzwa kuwa yadi ya kuuza magari.
Pia
alilalamikiwa kushitakiwa mahakamani na Marehemu Christopher Mtikila na watu
wengine watatu kwa kosa la kuwatishia silaha ya moto na kuwapapasa maungoni
mwao bila ridhaa yao kinyume na maadili ya kikanisa.
Askofu
Mokiwa pia analalamikiwa kuanzisha taasisi ya MEA Foundation iliyomwezesha
kupokea fedha nyingi za wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya dayosisi, lakini
fedha zimefujwa na hesabu za chombo hazikuwahi kukaguliwa.
Tuhuma
zingine ni kurejea kwa mchakato wa mapitio ya katiba mpya na kuvuruga mchakato
wa awali wa maandalizi ya katiba mpya ya dayosisi kwa kutumia fedha za dayosisi
na kutekelezwa askofu msaidizi dayososi ya Katanga Kalemi .
No comments