MAAFISA UVUVI WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.
Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (MAZINGIRA) na mwenyekiti wa kikao hicho Januari Makamba akizungumza na
waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Serikali katika kupambana
na uvuvi haramu nchini mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichohusisha Wizara
Saba kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo Pichani) athari za uvuvi haramu na jinsi unavyoathiri uchumi wa nchi kushoto ni Naibu Waziri aOfisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kutoa maagizo ya Serikali kwa wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kupambana na uvuvi haramu, kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na mwenyekiti wa kamati hiyo.
Dar es salaam
Serikali
imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi
kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa
kuzuia uvuvi haramu.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba Maliasili,
Ulinzi, Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya
Ndani Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia
agenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao.
Alisema
kuwa maafisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia
ni kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia
mabomu.
“Kuna
baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo
kuanzia kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu
atatolewa katika nyazifa hiyo”.
Kwa
upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema
kuwa nchi yetu inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na
changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka
katika kupambana na uharamia huo.
Akifafanua
zaidi kuhusu hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa
jambo la uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi
wa nchi hivyo lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa.
Alisema
ni aibu kwa taifa letu la Tanzania kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi
nyingi kwa sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.
Naye
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania
wote kushirikiana na Serikali katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi
haramu.
Mwigulu
Nchemba alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika
kulinda rasilimali za majini tulizo nazo”.
Kikao
hicho ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu
ambapo maazimio hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita
kwa ajili ya kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale
patakapoonekana pana changamoto
No comments