KUTOKA TARIME: MFANYABIASHARA AMTWAGA RISASI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU.
MFANYABIASHARA
Robert Mwikwabe, maarufu kama Ndugu, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kumpiga risasi ya kichwani na kusababishia kifo papo hapo mwanafunzi wa kidato
cha tatu wa shule ya sekondari Sirari, Masaite Mrimi(17).
Kutokana
na tukio hilo, Mwikwabe ambaye pia ni mmliki Hoteli katika mji mdogo wa Sirari
wilayani Tarime mkoani Mara, alinusurika kuteketezwa yeye na familia yake Hali
hiyo ilitokea baada ya wananchi kuamua kuchoma moto lori la mfanyabiashara huyo
na kwenda nyumbani kutaka kuchoma hoteli.
Mashuhuda
walisema tukio hilo ni la juzi mchana, jirani na nyumba anayoishi mwanafunzi
huyo, eneo la stendi mpya ya mabasi na malori ya Ngerengere.
Walisema
mfanyabiashara huyo alifika akiwa na lori lake likiwa na mawe na alisimama na
kutaka kuchukua pumba za mchele, zilizomwagwa na malori yanayosafirisha ng’ombe
kwenda nchini Kenya.
Eneo
hilo ni jirani na nyumbani kwao marehemu, ambako kulitokea mzozo kati ya Robert
na wazazi wa mwanafunzi huyo. Kufuatia mzozo huo, mwanafunzi huyo aliyekuwa na
panga mkononi, alimtishia kumkata Robert, ambaye alichomoa silaha yake aina ya
bastola na kumpiga risasi kichwani na kumsababisha kifo.
Baada
ya tukio hilo, familia ya marehemu na wananchi walianza kumfukuza Robert
aliyeacha lori lake likiwa na mawe na kukimbilia lori lake lingine la jirani.
Kisha alikimbilia Kituo cha Polisi Sirari, kuokoa maisha yake.
Umati
mkubwa wa watu kutoka vijiji vya Ngerengere na Sirari, walikwenda nyumbani kwa
mfanyabiashara huyo kwa lengo la kutaka kuchoma moto hoteli na nyumba.
Lakini,
polisi na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga walifanya juhudi kubwa
kuwazuia wananchi hasa vijana, kuacha kuteketeza mali za mfanyabiashara huyo
yakiwemo magari, ambayo sasa yamehifadhiwa kituo cha polisi kwa ajili ya
usalama.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Tarime-Rorya, Andrew Satta alithibitisha kutokea kwa
kifo cha mwanafunzi huyo na kwamba maiti imehifadhiwa katika hospitali ya
wilaya Tarime.
Chanzo-Habarileo
No comments