KINANA AZINDUA KAMPENI JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR KWA KISHINDO, AWANANGA CUF
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM,Andulrahman Kinana akimnadi Mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani Juma Ali Juma, katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo, mjini Zanzibar, Januari 5, 2017
Katibu
Mkuu wa CCMAbdulrahman Kinana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo
wakiwasalimia wananchi wakati Kinana akimtambulisha Mpogolo, katika mkutano wa
uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar.
Wananchi
wakipokea kwa furaha salama za Kinaa na Mpogolo walipowasalimia wakati wa
uzinduzi wa kampeni hizo
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akisalimia wananchi baada a
kutambulishwa na Kinana kwenyeuzinduzi wa kampeni hizo mjini Zanzibar
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wakati wa
uzinduzi wa kampeni hizo mjini Zanzibar
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Ali Seif Idi,
akizungumza na wananchi baada ya kukaribishwa a Kinana kwenye uzinduzi wa
kampeni hizo,jibola Dimani Zanzibar.
Katibu
wa NEC, Itikadina uenezi Humphrey Polepole akisalimia wananchi baada ya kukaribishwa
na Kinana kwenye uzinduzi wa kampeni hizo, jimbo la Dmani Zanzibar
Polepole akionyesha furaha
yake wakati akiwasalimia wananchi baada ya kukaribishwa na Kinana kwenye
uzinduzi wa kampeni hizo katika jimbo la Dimani, Zanzibar
Polepole
akizungumza baada ya kukaribishwa na Kinana kwenye uzinduzi wa kampeni hizo
jimbo laDimani .
Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu, Ngemela Lubinga, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM
za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar
Katibu
wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib akizungumza na wananchi
alipokaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa
uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani,
Zanzibar.
Wananchi
wakiwa na mabango kuonyesha walivyojitokeza katika uzinduzi wa kampeni hizo
(PICHA NA BASHIR NKOROMO).
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni zake katika jimbo la Dimani mkoa wa
mjini magharibi kisiwani Unguja na kukishangaa chama Cha wananchi (CUF) kwa kushindwa kutanua wigo wa
demokrasia ndani ya chama hicho na kuendelea kumshikilia mgombea mmoja wa urais
Zanzibar wa kudumu miaka kwa miaka .
Kimesema
wananchi wataendelea kukichagua chama hicho tawala kwa sababu ya kufuata misingi bora ya demokrasia, misimamo thabiti, sera
endelevu na utamaduni wake wa
kubadilisha wagombea .
Hayo
yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman
Kinana (pichani juu), wakati akizindua kampeni za CCM uchaguzi mdogo wa Ubunge
jimbo la Dimani, zilizofanyika katika
eneo la Maungani nje kidogo ya mji wa Unguja.
Kanali
Kinana alisema CCM itaendelea kuchaguliwa na wanqnchi kwasababu kinatimiza
wajibu wa kuwatumikia wananchi, kutikiza matakwa ya kisera na kushughulikia
matatizo na shida za wananchi.
"Demokrasia
ndani ya chama chetu ni ni ya aina yake na kwamba kukubalika kwetu mbekw ya wananchi nikutokana
na misimamo yetu inayotetea maslahi ya
umma na vile vile demokrasia ndani ya CCM haifanani na vyama vingine ",
Alisema Kinana.
Alisema
chama hicho kina umoja imara, hazuiwi mwanachama kuwania nafasi ya uongozi na
kwamba hakina sifa ya kuwa na wagombea wa kudumu kama kilivyo chama cha CUF
ambacho tokea kilipozishwa mwaka 1992 hadi sasa Katibu mkuu na mgombea
urais ni huyo huyo Maalim Seif Sharif
Hamad
Pia
Katibu mkuu huyo alisema kushiriki kwa
wagombea takriban 25 ndsni ya CCM waliowania nafasi ya ubunge jimbo la Dimani
na kupatikana mmoja huku akiungwa mkono na wenzake ni kieelezo tosha kuwa ndani ya chama hicho kuna umoja imara na demokrasia ya kweli.
Alieleza
kuwa vikao vya CCM vya Nec na kamati kuu
vimeketi kujafili hatimaye kupitisha jina la mgombea aliyeshinda kura za
maoni huku chama cha CUF kikiwa kimya na bila kufanyika vikao vya kikatiba.
Akizumgumzia
kupwaya kwa dhana na misingi yq demokrasia ndani ya CUF, Kinana alikipinda
chama hicho na kusema kuwa hivi sasa chama hicho kina wenyeviti watatu, mmoja
akiwa wa muda, mwingine wa mpito na aliyebaki ni wa zamani
"Kuna
mgombea mmoja hapa Zanzibar ameanza kugombea urais tokea akiwa na miaka 30 na
sasa ana miaka 80, toka akiwa bado kijana mbichi sasa amekuwa
kikongwe na kupinda mgongo ila bado ana tamaa ya kuwania urais"
Alisema Kinana.
Aidha
Kinana aliwashangaa wanachama wa CUF ambao wanakubali kudanganywa kirahisi kila
siku na kuaminishwa iko siku mgombea wao wa urais sliyeshindwa uchaguzi
atatangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Rais wa Zanzibar.
"Tuliambiwa
hapa uchaguzi mkuu wa Zanzibar utafutwa,
watakuja watu toka UN , mara tukaelezwa
wangekuja jumuiya ya ulaya, wakaambiwa
washone nguo mpya kusherehekea ushindi huku siku zikitaradadi hakuna
kinachotokea "Alieleza Kinana.
Hata
hivyo Kinana alisema chama cha CUF viongozi wake hawana uwezo wowote wa kuwatumikia wananchi na
kuwaletea maendelwo kwa maelezo kuwa walibahatika kuingia katika seikali ya
umoja wa kitaifa na kushindwa kufanya lolote.
"Kama
ni mkate CUF walipata nusu na CCM nusu,
wakashika Wizara makini za Biashara na Viwanda, Katiba na Sheria, Haabari na
Utamaduni, mawasiliano na miundombinu lakini kutokana na wao kuwa udhaifu,
hawakumudu hata kujenga kiwanda
kidogo"Alisisitiza
Katibu
Mkuu huyo wa CCM aliwaomba wananchi wa
Dimani kumchagua mgombea ubunge aliyesimamishwa kwa tiketi ya CCM Juma Ali Juma
kwasababu ni makini, mchapakazi na mwepesi wa kuwatumikia wananchi.
Akihutubia
Katika mkutamo hup wa uzinduzi wa kampeni, mjumbe wa kamati kuu ya ccm Balozi
Seif Ali Idd aliwaeleza wananchi wa jimbo la Dimani kuwa si sifa ya wagombea wa
CUF kuwatumikia wananchi na mfano mzuri ni katika majimbo ya pemba.
Balozi
Seif ambaye ni makamu wa pili wa Rais Zanzibar, alisema viongozi wa chama hicho
hawana uzoefu wala historia ya kuwatumikia wananchi katika majimbo yote
walibahatika kushinda "Alieleza Balozi Seif.
"Sifa
ya kuwatumikia wananchi ni ya ccm na viongozi wake,yatazameni majimbo ya Pemba,
Mji Mkongwe na Nungwi, yako taaban kwasababu wawakikshi waliochaguliwa hawana uwezo na dhamira ya
kuwatumikia watu "alieleza Balozi Seif.
Kwa
upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa mwemvuli wa ccm Juma Ali Juma
alisema amejipanga kuwawakilisha wananchi ipasavyo, kuwatumikia, kushirikiana nao na kuhakikisha
ilani ya uchaguzi ya ccm inatekelezwa hatua kwa hatua.
Katika
mkutano huo wa uzinduzi umehudhuriwa na
mke wa makamu wa pili wa Rais Mama Asha Suleiman Idd, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa Itikadi na Uenezi Hamperey Polepole na
Katibu wa Oganaizeshaeni Dk Mohammed Seif Katibu , Spika Mstaafu wa baraza la
wawwkilishi zanzibar Pandu Amir Kificho na mwenyeliti wa ccm mkoa wa Mgjaribu
Yusuf Mohammed Yusuf.
No comments