UKARABATI WA RELI KUPUNGUZA SAFARI ZA TRENI YA JIJI KUTOKA DAR KWENDA PUGU KUANZIA 2 JANUARI 2017
Kampuni
ya reli nchini (TRL) imetangaza kuanza kufanya
maboresho ya reli yake kwa kiwango cha ratili 80 kutoka kituo kikuu cha
Dar es salaam mpaka Pugu kuanzia jumatatu ya januari 2 mwaka 2017.
Akizungumza
mapema leo jijini dar es salaam, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji wa kampuni
ya Reli nchini (TRL) Ndugu Focus Sahani alisema kuanza kwa mradi huo wa
kutandika reli za uzito wa ratili 80 na kuondoa zile nyepesi za ratili 60
kuanzia Kituo kikuu cha Dar es Salaam mpaka Pugu umbali wa kilomita 20.4 umelenga
kuboresha utoaji wa huduma za usafiri huo kwa ufanisi zaidi.
Amesema
kuanza kwa ukarabati wa njia hiyo ambao utachukua takribani wiki 10 mpaka
kukamilika kwake utapelekea kupunguzwa safari 2 za treni ya Jiji kwenda
Pugu ambazo ni Safari ya mwisho asubuhi ya
3:15 na ile ya mwisho usiku saa 2:45,
Aidha
amezitaja Faida itakayopatikana baada ya
kazi hiyo ni reli kuimarika ni kupunguza kutimka vumbi kama ilivyo sasa wakati
treni ikiwa inatembea na kuongeza
kuwa Kokoto zitakazotumika katika ujenzi
huo ni maalum hazitoi vumbi wakati treni ikipita.
No comments