SIRI YA RAIS MAGUFULI KULA CHRISTMASS MKOANI SINGIDA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali
Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.
Ametaja
siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali
kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki
jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi
huo.
Rais
Magufuli ametoa siri hiyo jana wakati
akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya
Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.
Akifafanua,
alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa
siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.
“Hiyo
ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi
wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu
kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.
Rais
Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya
Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia
hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.
Katika
hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe
wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo
kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.
“Ndugu
zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea …
fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya
madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya
kazi na asile,” alisisitiza.
Akiijengea
nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi
mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania
wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.
Aidha,
Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao
la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha
Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.
Awali
askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo
kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza
na wao.
Alisema
hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu
mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.
“Mimi
nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na
kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu
wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”,
alisema Mapunda.
No comments