SHEIKH JALALA ATUMA SALAM ZA KHERI NA FANAKA YA KUZALIWA YESU KWA WAKRISTO WOTE
TAARIFA
KWA UMMA
Amani ya Mwenyezimungu iwe juu yenu nyote.Salam hizi za
Mkono wa Krismas kwa ndugu zetu Wakristo wa Tanzania na Wakristo wote
wanaosheherekea Mazazi (Kuzaliwa) kwa Nabii Issa (a.s) Mtume wa Mungu kwa ndugu
zetu wakristo ni Yesu Kristo.
Mkono huu wa Kristmass, Mkono huu wa Eid ni Mkono uliobeba
Umoja, ni mkono uliobeba Mshikamano ni Mkono wa Eidi, ni mkono wa Krismaa
uliobeba amani na Maelewano. Lakini kubwa zaidi la kujiuliza na huenda wengi
wakajiuliza swali hii kwamba kwanini Viongozi wa Dini wa Kiislam katika siku
hii ya kuzaliwa Yesu Kristo au Nabii Issa (a.s) kwa Wiaslam, viongozi hawa wa
Kiislam hususan Wafuasi wa Madhehebu ya Ahlulbayt (a.s) au Mashia watoe Mkono
wa Krismas,mkono wa kheri,
mkono wa Baraka kwa ndugu zao wakristo Watanzania na wa Dunia
kwa ujumla ni kwasababu chache za harakaharaka nitakazozieleza
Sababu ya kwanza tutambue sisi Waislam na ndugu zetu
Wakristo sote tunakusanywa na neon moja kwamba sisi ni Waumini,
sote tunamuamini Mungu mmoja ambae ndie aliyeumba Mbingu na
ardhi na akawaumba wanadam wote hilo la kwanza, Sote tunaamini kwamba kuna
vitabu vya Mungu vilivyoshushwa hapa duniani, tunaamini uwepo utumwa mitume wa
Mungu na vilevile tunaamini siku ya mwisho.
Kwahivyo kuyaamini haya yanatukusanya sisi watanzania
Waislam na Wakristo chini ya mwamvuli mmoja wa imani, kwahivyo leo hii waislam
tunapotoa mkono wa Krismas, mkono wa eid kwa ndugu zetu wakristo ni kwasababu
ni waumini wenzetu katika kumuamini Mungu mmoja, katika kuamini siku ya mwisho
na katika kuamini mitume waliotumwa na kutuletea ujumbe hili la kwanza.
La pili kwanini mkono wa Krimsaa kwa ndugu zetu Wakristo, ni
kwasababu sisi wote tunakusanya na anuani ya Utanzania, Waislam tulioko hapa ni
Watanzania, wakristo tulioko hapa ni Watanzania, kama sote ni watanzania ni wajibu
wetu sote kuilinda Tanzania yetu. Kama sisi Wislam na Wakristo ni Watanzania ni
wajibu wetu umoja na mshikamano wetu kama Watanzania, kama sisi sote ni
watanzania ni makosa makubwa kufungua mwanya wowote wa mvutano kati ya Waislam
na Wakristo hapa Tanzania, kwanini kwa sababu sote tunakusanywa ni Utanzania.
Kwasababu sisi sote ni watanzania ni lazima tuwe na sifa ya
kuvumiliana, itikadi zetu, fikra zetu na mitazamo yetu isitugawanye kwa kuwa
sisi tunakusanywa na neon Utanzania,Na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa sisi
waislam anasema “kupenda inchi yako ni katika imani” kwahivyo leo hii sisi kama
Viongozi na kama Waislam na kama Waislam Shia Ithnasheriya tunapotoa Mkono wa
Krisma, mkono wa Baraka na mkono wa Eid kwa ndugu zetu Wakristo moja ni kuenzi
huu Utanzania tuliokuwanao ambao ni kitu muhimu na ni kitu kikubwa,Lingine ni
kwanini tunatoa mkono wa Krismas,
ni kwasababu sisi Waislam, Dini ya Uislam ni dini ya
Mapenzi, Dini ya Uislam ni dini ya kufahamiana, Dini ya Uislam ni dini ya
amani, Dini ya Uislam ya kupendana, anaeueleza Dini ya Uislam sio dini ya
kupendana huyo hajauelewa Uislam.
Kwahivyo Uislam ni dini ya Mapenzi, ni dini ya Maelewano ni
dini ya Maelewano,Mtume Muhammad (s.a.w.w) anatufunza siku zote anasema “ penda
watu wapate kile ambacho unachopenda ipate nafsi yako” kwahivyo Uislam ni dini
ya upendo, uislam ni dini ya Maelewanoni dini ya masikilizano leo hii tunapotoa
mkono wa Baraka na mkono wa kheri na fanaka katika Eid ya Krismass malengo
makubwa ni kuwaonyesha ndugu zetu wakristo kwamba Uislam ni dini inayompenda
kila mtu, Uislani dini iliyohimiza ujirani mwema na ujirani huu mwema hauwezi
kudhibitika wala kufanyika pasi na watu kupendana.
Kwahivyo mkono huu wa Krismass ni mkono wa kuwaonyesha ndugu
zetu Wakristo Wayanzania kwamba Uislam ni dini ya mapenzi, kwamba uislam ni
dini ya kuelewana, Sayyidina Ali (a.s) kiongozi baada ya Mtume Muhammad
(s.a.w.w) anawausia watoto wake anawambia “Hala hala nawahusieni majirani”
Sayyidina Ali (a.s) alipokuwa anawahusia watoto wake swala la Majirani, hajawaambia
Majirani Waislam, hajawaambia Majirani wachamungu la, kawaambia Majirani yaani
majirani wote ima wachamungu, Wakristo, Waislam na hata wasiokuwa na Dini.
Kwahivyo kitendo cha leo cha sisi kutoa Mkono wa Krismass,
mkono wa Kheri na Baraka kwa ajili ya ndugu zetu watanzania wasiokuwa Wiaslam
ni kutaka kuwaonyesha kuwa Uislam ni dini ya mapenzi uislam ni dini ya
maelewano.Nukta nyingine muhimu kwanini Mkono wa Krismass,mkono wa Kheri na
Baraka kwa ndugu zetu Wakristo kwa sababu hakuna uadui kati ya Uislam na
Ukristo, hakuna Uadui kati ya Waislam na Wakristo,
Ukimsoma Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ukiisoma Qur’an yetu na
ukisoma mwenendo wa watu waliokuja baada ya mtume Muhammad (s.a.w.w) utapata
yakwamba wanavyoueleza Uislam, Uislam na Ukristo sio uadui kati yao bali ni
Udugu na maelewano kati yao.
Iangalie Qur’an inavyowasemesha Wakristo inawaitaje,
inawaita “Ahlul Kitabu” enyi watu waliopewa Injili, enyi watu mliopewa Taurat,
enyi watu mliopewa Zaburi hivi ndivyo Qur’an inavyowasemesha Wakristo, kwahivyo
Mkono huu wa Kheri na Baraka ni kuonyesha ya kwamba hakuna Uadui hata kidogo
kati ya Uislam na Ukristo, kati ya Waislam na Wakristo.
Ukiisoma Qur’an, Qur’an ina sura nzima inayoitwa suratul
Mariam yaani sura ya Mariam, mariam ambae kwa ndugu zetu Wakristo wanamwita
“Bikira Maria” sisi kwetu Waislam tunamwita “Mariam Mtakatifu” ni sura nzima
inayobeba jina la Mariam, kwahivyo lau Uislam ungelikuwa na Uadui na Ukristo
kusinge kuwa na sura inayoitwa sura ya Maria.
Vilevile ndani ya Qur’an kuna sura ya Ruum yani sura ya
Roma, Roma ni Wakristo ndani ya Qur’an, na Waislam wanaisoma sura hiyo kila
siku ya asubuhi na mchana
Mwisho nimalizie kwa nukta yakwamba Kitendo cha sisi kutoa
Mkono wa Kheri ya Krismass kwa ndugu zetu Wakristo watanzania ni kuonyesha
yakwamba Uislam ni dini ya Amani, Uislam ni dini inayopenda watu wakae vizuri,
Uislam ni dini inayopenda mahusiano mazuri kati yao na ndugu zao Wakristo,
na kwamba Uislam katika vitu inavyovipiga vita ni kitu
kinachoitwa Ugaidi, Uislam na Ugaidi ni vitu viwili tofauti, ni kuontesha ya
kwamba Uislam hauna kitu ukatili kwa wasiokuwa Waislam
Kitendo hiki cha kutoa mkono wa Krismas kwa ndugu zetu
Wakristo ni kuonyesha kwamba Uislam hauna chinja chinja kwa Wakristo, Uislam
hauna ukatili kwa Wakristo,
Uislam ni amani na maelewano kwa Waislam na wasiokuwa
Waislam.mwisho niwatakie ndugu zetu wakristo Watanzania Eid njema, Krismass
njema ya kusheherekea kuzaliwa Yesu Kristo au Nabii Issa (a.s).
Na vilevile ni itakie amani serikali yetu ya awamu ya tano
ambayo imeweza kutufikisha hapa kwa utulivu na kwa maelewano sisi Waislam
Watanzania na Wakristo wa Tanzania, na ninamuomba Mwenyezimungu Serikali hii
awape hekima, awape busara ili waendelee kutuongoza kwa salama na kwa amani na
vilevile mwenyezimungu nchi hii azidi kuboresha maelewano
kati yetu sisi Waislam na kati ya ndugu zetu Wakristo, na yeyote ambae anania
ya kuleta chokochoko ya kuvunja amani hii, basi chokochoko yake isiweze kuingia
katika nchi yetu ya Tanzania na katika taifa hili, Mungu azidishe kulibakiza
Taifa hili la Tanzania katika Amani na kisiwa cha amani na mahala pa
maelewano.Asanteni sana na Mungu awabariki.
Imetolewa
Na:
Kiongozi
Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
No comments