SAKATA LA ALIYEKUFA MUDA MFUPI BAADA YA KUBATIZWA KIKRISTO, AZIKWA KIISLAM
Kijana Issa Juma aliyeripotiwa kufariki dunia Jumapili
iliyopita, muda mfupi baada ya kubadili dini na kubatizwa katika mto mmoja kwa
imani ya Kikristo akijiunga na kanisa la Efatha kwa jina la Paulo, amezikwa kwa
imani ya Kiislam.
Uamuzi huo umefikiwa
baada ya kuwepo mvutano kati ya Kanisa la Efatha na viongozi wa dini ya Kiislam
wakitaka kijana huyo azikwe kwa imani yao, lakini mwisho kauli ya wazazi wa
marehemu ilikuwa na nguvu zaidi na hivyo kuzikwa kwa imani ya Kiislam.
Akizungumzia uamuzi
huo, mama mdogo wa marehemu ambaye jina lake halikupatikana alizungumza kwa
niaba ya mama mzazi, Rehema Juma alithibitisha kuwa walimzika ndugu yao Jumanne
wiki hii kwa imani ya Kiislam.
Kifo cha kijana huyo
kiliibua sintofahamu ikiwa ni saa chache baada ya kuzaliwa kwa mara pili kwa
imani ya Kikristo na haikufahamika mara moja chanzo chake kama alikuwa na
ugonjwa ama ni masuala ya kiiman
No comments