Breaking News

RAIS MAGUFULI AMETOA OMBI KWA WATANZANIA KUELEKEA MWAKA MPYA 2017

Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wote kuutunza na kuudumisha umoja katika mwaka 2017 huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii.

Rais Magufuli amendika maombi hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo pamoja na kuwaomba Watanzania kutekeleza mambo hayo amewatakiwa Watanzania heri ya mwaka mpya.

“Ombi langu kwa Watanzania wote tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA,” ameandika Rais Magufuli.
Ombi langu kwa Watanzania wote tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Watanzania wenzangu,tukiwa tunakaribia kuumaliza mwaka 2016,naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya 2017.

No comments