MAJINA YA WALIOKUWA WAMEFAULU USAILI WA AJIRA SERIKALINI, KUFUTWA.
Watu
wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia
Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa,
watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo
zitakapotangazwa tena.
Hilo
limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali kwa
mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila mwezi kupitia
tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale ambao walifaulu
usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au kupewa barua na waajiri
wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa.
Taarifa
hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba
majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi
miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.
"Kwa
mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji
kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye
kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita" Imesema taarifa hiyo
Swali
lingine kutoka kwa mdau na jibu lake liko kama ifuatavyo:-
Kwa
kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni mwezi Desemba, utaratibu huo
unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini hawakupangiwa kazi,
watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na kufanya usaili upya.
Aidha
Sekretariet hiyo imebainisha kuwa zoezi ya uhakiki wa watumishi hewa bado
linaendelea, na kwamba wakipewa ruhusa ya kutangaza ajira wakati wowote
watatangaza.
No comments