KUTOKA MKOANI MBEYA: AMUUA RAFIKI YAKE....... ALA UBONGO WAKE NA SEHEMU ZA SIRI
JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia mchimba dhahabu, Shija Salum (38), mkazi
wa Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake na kula ubongo
wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa habari
jana kwamba pamoja na mtuhumiwa huyo kula ubongo wa rafiki yake huyo
aliyetambuliwa kwa jina moja la Shija, pia alitafuna sehemu zake za siri baada
ya kuzikata.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu,
usiku katika Kijiji cha Manyanya, Kata ya Makongorosi, Wilaya ya Chunya mkoani
Mbeya.
Alisema
mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi mitatu
iliyopita.
“Inasemekana
wawili hao walikuwa ni marafiki kwani walifika wilayani Chunya, Kata ya
Makongolosi kwenye machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja
aitwaye Teddy Mwantega.
“Siku
hiyo ya tukio, marehemu Shija, alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo alipofika
rafiki yake huyo, akiwa na panga mkononi na kumkata kwa nguvu kichwani.
“Baada
ya hapo, alimvua nguo na kuzikata sehemu zake za siri na kuzishika mkononi.
“Wakati
akiwa na sehemu hizo za siri mkononi, alichukua ubongo wa marehemu na kuula,
kisha akatafuna zile sehemu za siri.
“Kwahiyo,
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” alisema
Kamanda Kidavashari.
|
No comments