HAJI MANARA WA SIMBA AMWOMBEA MSAMAHA JERRY MURO TFF
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara
amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili
kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.
Jerry
Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na
TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya
ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.
Manara
katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais
wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni
wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa
kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo
linamuhitaji sana kwa sasa.
"Nimekaa
nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF
mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua
kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,
ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa
fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika
Manara
Manara
pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye
mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu
pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale
yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na
washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha
uungwana tulio nao wanasimba".
manara
amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na
kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado
alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.
Kwa
upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara
anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka
Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji
Manara.
No comments