Breaking News

BENKI YA NMB YAZAMINI MKUTANO WA SIKU MBILI WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN)




Mwenyekiti wa muda wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) kuhusu mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu wa TBN,Khadija Khalili na Mwisho kushoto ni Meneja wa Mitandao wa NMB, Joyce Nsekela.

Na Frank Wandiba
Waziri wa Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa siku mbili wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN)  utakaofanyika tarehe 5 na 6 mwezi huu katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa muda wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi alisema mkutano huo ambao utawakutanisha wanachama wapatao 150 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Alisema katika mkusanyiko huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine. 

"Mkutano huu umelenga kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji" alibainisha.

Alisema baadhi waendeshaji wa Mitandao ya kijamii kuifanya kazi hiyo kama ajira nyingine, na ukidhingatia kuwa mitandao ya kijamii imekuwa tegemeo kubwa katika kuripoti habari mbalimbali na kuwafikia walengwa kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio.

Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

Mkutano huo wa aina yake tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini, umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola.

No comments