Breaking News

SHEKH JALALA: TUMUENZI MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KWA KUTENDA HAKI, NA KUWA NA HURUMA KWA WATU WOTE BILA UBAGUZI


 Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam.
 Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA akiwaongeza mamia ya waumini wa dhehebu hilo katika matembezi ya amani kuadhimisha kifo cha Kiongozi wa waislam Mtume Mtume uhammad (s.a.w.)

Mamia ya waumini wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA wakishiriki matembezi ya amani kuadhimisha kifo cha Kiongozi wa waislam Mtume Mtume uhammad (s.a.w.) mapema leo jijini dar es salaam.

Na Frank Wandiba
Watanzania wametakiwa kuunda Umoja wa Dini zote ambazo zitawaunganisha Waislam, Wakristo, Wayahudi na Wapagani iwe ni moja ya Mikakati ya Kumuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika kudumisha Amani.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam katika Matembezi ya Amani ya Kuomboleza na kukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W.W), kiongozi Mkuu wa Waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala kwa kufanya hivyo watakuwa wanatekeleza moja ya mafunzo ambayo alikuwa hakitoa wakati wa uhai wake.

Alisema viongozi wa dini Masheikh,Maimam, wachungaji, maaskofu, mapadre na viongozi wa madhebu mengine ya dini mbalimbali kuondoa tofauti zao hili kujenga umoja na mshikamano na kuiga huruma ya Mtume Muhammad s.a.w. 

Aidha shekh jalala aliongeza kuwa katika Miaka 1400 iliyopita tangu kifo chake  Mtume Muhammad S.A.W alikuwa kiongozi ambaye alitenda haki na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana.

Matembezi hayo ya Amani ya kukumbuka kifo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki tarehe 28, Safar, Mwaka wa 11 AH, yaliyobeba Ujumbe "Mtume Muhammad (S.A.W.W) ni Rehema kwa watu wote, yalianzia Ilala Boma hadi Uwanja wa Pipo Kigogo, Dar es salaam., 


No comments