Breaking News

MAUZO YA HISA KATIKA SOKO LA HISA LA DAR (DSE) YASHUKA KWA ASILIMIA 37

Idadi ya mauzo imeshuka kwa asilimia 37% na kufikia TZS 4 Bilioni kutoka TZS 6.4 Bilioni wiki iliyopita.

kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa mauzo wa soko hilo ya wiki iliyoishia 18 Novembar imesema kuwa Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imeshuka kwa asilimia (94%) hadi laki 671,618 kutoka Milioni 11,065,589 wiki iliyopita.

Pia taarifa hiyo imebainisha kuwa Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni bank ya CRDB kwa asilimia 42.40%, TBL kwa asilimia 41.44%, DSE kwa asilimia 6.44%

Kwa pande wa Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 2.4% na kufika Trilioni 20.9 kutoka Trilioni 21.4 wiki iliyopita.

Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umeshuka kwa wastani wa asilimia 0.6% hadi Trilioni 8.14 kutoka Trilioni 8.19 wiki iliyopita.

Aida tarifa hiyo imeongeza kuwa Viashiria (Indexes) Sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kupungua kwa pointi 40.84 baada ya bei ya hisa za TCCL na TBL kupungua kwa asilimia 13.98% na 0.74%.

huku ikifafanua  kuwa Sekta za Huduma za Kibenki na Kifedha wiki hii ilibaki kwenye wastani ule ule wa Tzs 2,771.18  sambamba na Sekta ya Huduma za Kibiashara nayo wiki hii ilibaki kwenye wastani ule ule wa Tzs 3,157.95.

No comments