SAKATA LA CUF LACHUKUA SURA MPYA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA PROF LIPUMBA WAFUNGULIWA SHAURI MAHAKAMA KUU DAR.
Wakili
Juma Nassoro akizungumza na waandishi mara baada ya kufungua shauri hilo leo
mahakama kuu, kanda ya Dar es salaam
Na
Frank wandiba
Bodi
ya wadhamini wa chama cha wananchi (CUF) leo imefungua shauri Namba 75 , 2016
katika mahakama kuu, kanda ya Dar es
salaam dhidi ya msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, Mwanasheria
mkuu wa serikali , Profesa lipumba pamoja na wenzake 12 waliosimamishwa
uanachama wa chama hicho.
Kiongozi
wa jopo la mawakili wa CUF watakaosimamia kesi hiyo wataongozwa na Juma Nassoro
alisema shauri hilo limefunguliwa na kwamba linatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi oktobar 10, 2016.
“Bodi
ya udhamini ya Cuf imefungua shauri hilo dhidi ya Jaji Mitungi na wenzake 12 waliosimamishwa uanacham,a pamoja ba
Lipumba” Alisema.
“
Tunaitaka mahakama iende mbali zaidi ,
itoe amri ya kumzuia msajili kufanya shughuli ambazo zipo nje ya mamlaka
aliyopewa na sheria ya vyama vya siasa , ili kuendelea kuimalisha democrasia na
msajili kufanya shughuli zake kwa mujibu washeria.’
Bw
Nassoro aliongeza kuwa wajumbe saba wa bodi ya uwadhamini cuf ambao msajili wa
vyama vya siasa ambao amedai kuwatambua ndio waliofungua shauri hilo leo.
“Wajumbe
waliokuja kwangu ni saba majina yao sina kwa sasa ,hao wengne ambao wamekuwa wakifanya
vikao katika ofisi za chama hicho zilizopo buguruni sio sahihi hivyo mwisho wa siku amhakama ndio
itatoa tafsiri Bodi hipi sahihi na uongozi upi sahihi” alisema
No comments