Breaking News

KIWANDA CHA WACHINA DAR CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI ISHIRINI NA TANO KWA KUKIUKA SHERIA YA MAZINGIRA NA KAUNI ZAKE

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.    
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.

 Dar es salaam

Kiwanda cha kutengeneza mifuko maarufu kama viroba cha UNBERG INTERNATIONAL cha jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Raia wa China kilichopo katika eneo la viwanda Mandela Road jijini Dar es salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kukiuka vibaya sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Kiwanda ambacho kilikuwa hata hakijulikani kinachotengeneza mifuko itumikayo kufungia bidhaa mbali mbali kama sabuni, saruji na sukari, kimeonekana kufanya kazi ya uzalishaji katika mazingira hatarishi kwa wafanyakazi kiwandani hapo pamoja na mazingira.

Hayo yamebainika katika siku ya pili ya hitimisho ya ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu waRaisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpiga alipokua akikagua baadhi ya Mazingira ya jiji la Dar es Salaam na viwanda, ndipo alipoingia kiwan dani hapo kwa kushtukiza na kujionea namna ambapo raia hao wa China wanavyotiririsha uchafu wa kinyesi cha binadamu katika mto msimbazi.

Naibu Waziri Mpina alisema, “Tunawapenda na kuwajali wawekezaji ila kwa Uchafuzi huu mnaoufanya hapa hata kama ingekuwa nchini kwenu hii isinge ruhusiwa, nilitaka kiwanda hiki kifungwe kabisa lakini lazima taratibu za kisheria zifuatwe. Kiwanda hakina hata cheti kimoja kinachowaruhsu kuanya kazi hizi” Alisisitiza Mpina.  Pamoja na uchafu wa maji baada ya kuswafisha malighafi ya mifuko hiyo kiwandani hapo ambayo nimifuko ya bidhaa mbali mbali ikirejelezwa bila kujali wala kutibu maji na kuyaachia katika mazingira.

Akitaja adhabu katika kiwanda hicho mratibu wa kanda ya mashariki kutoka baraza la taifa  la hifadhi na usimamizi  wa mazingira NEMC Bw. Jafari Chimgege, amesema kuwa kiwanda kinatakiwa ,kulipa faini hiyo ndani ya siku saba na kuacha kutiririsha maji pamoja na kurekebisha wa usafishaji viroba kiwandani hapo, kupata cheti chatathmini ya athari za mazingira pamoja na vibali vingine vya uwekezaji nchini.

Kwa upande wake mtaalam wa maji Ardhini kutoka bonde la Wami Ruvu Bw. Msuda,amewataka wawekezaji na wenye viwanda nchini kufika katika ofisi za Bonde zilikzopo Ubungo maji jijini Dar es Salaam  ili waweze kufanya mchakato wa kupata vibali na vyeti vya kutiirisha maji machafu yaliyotibiwa kwa njia sahihi.

Naibu waziri mpina amehitimisha ziara yae ya siku mbili jijini Dar es salaam ya kukagua baadhi ya viwanda na mazingira.


 


No comments