Dar
es salaam
Ikiwa maadili ya uongozi
nchini bado ni changamoto wanazuoni wanatarajia kukutana na kujadili miiko ya
uongozi na azimio la Arusha Octoba 14 katika ukumbi wa chuo cha kumbukumbu cha
mwalimu Nyerere ili kuweza kuwakumbusha wajibu wao katika jamii.
Akizungumza na waandishi
jijini Dar es salaam Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila
amesema wameandaa kongamono kwa lengo la kumhenzi hayati mwalimu Nyerere na
kuchambua mada mbalimbali walizozichagua siku hiyo.
Profesa Mwakalila amesema
kuwa kongamano hilo litafanyika siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17
ya kifo cha Baba wa Taifa ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Miiko ya
uongozi na Azimio la Arusha”pia wananchi wataweza kujua kinachoendelea katika
azimio la Arusha.
Aidha amesema maadili basi
yanachangamoto kwa kulitambua hilo wamewaarika wanazuoni watano ambao wayaweza
kuchambua mada ya Azimio la Arusha na maadili ya uongozi.
“Tumemwalika Dkt Harun
Kondo atakaye chambua Azimio la Arusha, Wilson Mkama na Mzee Joseph Butiku
watachambua Miiko ya uongozi pamoja na Ibrahim Kaduma na Mhe Philip Mangula
watakaojadili maadili ya viongozi,” amesema Prof. Mwakalila.
Hats hivyo Prof.
Mwakalila amesema kuwa Miiko ya uongozi na maadili ya viongozi wa Umma
ilisisitizwa na Mwalimu mara baada ya Uhuru na baadaye kusisitizwa zaidi katika
Azimio la Arusha la mwaka 1967.
Anna John ni mmoja wa
wananchi ameelezea umuhimu wa kongamano hilo kuwa wamefanya kitu kizuri ambacho
kitaweza kuwakumbusha viongozi waliojisahau katika uongozi wao na kuweza
kukumbuka alichokuwa anakisisitiza hayati mwalimu nyerere katika enzi yake.
" Naimani wanazuoni
hao watatukumbusha mengi ili tuweze kukumbuka yale yaliyosaaulika"amesema
|
No comments