PROF. NDALICHAKO AMETOA SIKU SABA KUANZIA AGOSTI 17, 2016 KWA VYUO VIKUU KUREJESHA FEDHA ZA WANAFUNZI HEWA.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
Na
Frank wandiba
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku
saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo
ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.
Prof.
Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika
wa mikopo vyuo vya Elimu juu.
Prof.
Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati
ya vyuo 81 vilivyopo nchini.
Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.
Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.
“Mikopo
ya Wanafunzi hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini
walishindwa kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua
Mhe. Ndalichako.
Ameendelea
kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu
Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460.
Kutokana na mambo yaliyobainika Serikali imechukua hatua
zifuatazo
Vyuo
vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa
virejeshe fedha hizo ndani ya siku saba kuanzia August 17 2016
Vyuo
vya elimu ya juu vinaagizwa kuweka mfumo mzuri wa uhifadhi wa kumbukumbu za
wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za
akaunti za benki ambapo fedha za mikopo hilipwa.
Vyuo
vikuu vinaagizwa kuwasilisha bodi ya mikopo, kwa wakati taarifa zote za
kitaaluma na za kibenki za wanafunzi ili kuiwezesha kufanya marekebisho stahiki
katika kumbukumbu zao na kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Bodi
ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za
wanafunzi kama zilivyopelekwa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa
wanafunzi wasiostahili.
Hatua
kali za kinidhamu zichukuliwe na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za
waafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa
wanafunzi wasiostahili.
Vyuo
viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa wanufaika wa mikopo ili kuepuka
kufanya malipo kwa wanafunzi hewa.
Wakuu
wa vyuo ‘VCs’ na Principals’ waweke mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya
wanafunzi yanayotumwa bodi ya mikopo na watawajibika kwa usahihi wa taarifa
zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaini kuwepo kwa usdadanganyifu
mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi; wapo ambao hawakufanya mtihani au waliofeli
lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mikopo.
Uchunguzi
zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambazo
zimelipwa kwa watu wasiostahili. Hatua hii inatokana na matokeo ya uchunguzi
ambao umebaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi waliohitimu tangu mwaka 2013
lakini wameendelea kupokea fedha na wengine waliofukuzwa kwa kushindwa masomo
tangu mwaka 2013/14 lakini bado wamelipwa hadi mwaka 2015/16.
No comments