SERIKALI KUTENGA BIL.15 KUKUZA UJUZI WA VIJANA NCHINI.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na
Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika
uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na
Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa
kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika
uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto
wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa
kwanza kushoto akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Dkt.Hamis Mwinyimvua wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki
wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali
nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana
,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa
Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili
kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.
Akizungumza kwa
niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa
Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge,
Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali
imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa
madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.
“Tunatambua
vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan
chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga
bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.
Aidha Mhe.
Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha
wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi
wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.
Kwa upande
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw.
Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia
upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi
kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa
uchumi wa nchi.
Naye
Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo
haja ya watanzania hususani wakulima
washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia
60 ya watanzania ni wakulima.
Mkutano huo
wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza
la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi
ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na
kumalizika 22 Julai mwaka huu.