ULINZI VITUO VYA DART KUIMARISHWA
Baadhi ya abiria wanaotumia
usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia
kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea
katika baadhi ya vituo hivyo.
Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara
mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya
vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea
abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.
Aliongezea kuwa walinzi wa kituo
hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu
yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.
“Tunashangaa hawa walinzi
wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa
nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui
wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.
Nae Bi. Herrieth Shangaa
aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo
hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja
hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema
kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo
wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa
kidigitali wa kudhibiti wahalifu
Mradi wa mabasi yaendayo haraka
ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya
foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni
miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa sana.
No comments