PROF. MAKAME MBARAWA ATOA MIEZI MITATU BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati),
akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY
LIMITED anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED
anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6, alipokagua maendeleo ya
ujenzi huo
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Kampuni ya
SINO HYDRO COMPANY LIMITED inayojenga Barabara ya Dodoma-Mayamaya kwa
kiwango cha Lami kuhakikisha barabara hiyo inakamilika.
Akizungumza mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yeye urefu wa kilomita 43.6 Prof.
Mbarawa amemtaka mkandarasi kuikabidhi barabara kwa Serikali ifikapo
mwezi Oktoba mwaka huu.
“Hakikisheni barabara hii ambayo
ni sehemu ya barabara kuu ya Great North Road inakamilika ili
kuharakisha mkakati wa Serikali wa kukamilisha barabara hiyo eneo la
Tanzania kwa kiwango cha lami, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Barabara ya Dodoma-Mayamaya ni
sehemu ya Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye urefu wa Kilomita 247.8
ambayo ujenzi wake umegawanywa sehemu tatu ambazo ni Dodoma-Mayamaya KM
43.6, Mayamaya-Mela-Bonga KM 188.15.
‘Kukamilika kwa barabara hii
ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Great North Road inayoanzia Capetown
Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri kutachochea fursa za kibiashara
na kiuchumi katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) na nchi za Kaskazini mwa Afrika’, amesisitiza Prof. Mbarawa
Mpaka sasa takribani shilingi
bilioni 43 zimeshalipwa kwa mkadarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED
kukamilisha kilimilisha KM 8 zilizobaki katika sehemu ya
Dodoma-Mayamaya, barabara ambayo ambayo imejengwa kwa viwango
vinavyokubalika.
Barabara ya Great North Road
inayopita mikoa ya Iringa, Dodoma na Arusha inaanzia Capetown Afrika
Kusini hadi Cairo Misri mbapo kukamilika kwake kutaliunganisha Bara la
Afrika kwa Barabara ya Lami.
No comments