Breaking News

JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA TEMEKE YAPEWA MSAADA WA KOMPUTA

Na Mwandishi wetu - Viongozi wa Jumuiya ya wazazi kupitia Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Temeke, Leo April 13 2025 wamekabidhiwa kompyuta mpakato (laptop) Ili kuwawezesha kufanya kazi zao kidijitali na kuendana na Dunia ya sasa.

Kompyuta hizo zilikabidhiwa kwa viongozi wa kata 23 katika zoezi la kuhitimisha wiki ya Wazazi Kiwilaya kwa kufunga Semina ya Uongozi na Mafunzo ya Tehama kwa Wenyeviti, Makatibu na Makatibu Emma wa Kata hizo za Wilaya ya Temeke. 
"Katika kuhitimisha wiki ya wazazi kiwilaya tunawakabidhi vitendea kazi hivi Ili mkafanye kazi kidigitali katika kutafuta kura za ushindi wa CCM kwa kishindo," alisema Slim

Katika hatua nyingine Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Slim walitembelea katika Kata ya Mtoni ili kujionea maendeleo ya miti iliyopandwa katika maadhimisho ya mwaka jana.
"Tumekuja kutembelea miti hii ambayo tulipanda mwaka jana, kiukweli tumeridhishwa nayo," alisema Slim.