Breaking News

CLOUDS KUPITIA KPINDI CHA SENTRO BASH WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA KUTIMIZA MIAKA 65

Na Mwandishi Wetu - Kituo cha luninga cha Clouds TV kupitia Kipindi chake cha Sentro Bash la Bimdash wameungana na watanzania kusherehekea kumbukizi ya tarehe ya kuzaliwa kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyetimiza umri wa miaka 65 January 27, 2025. 

Wakizungumza kupitia kipindi hicho Uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group umesema kupitia kipindi hicho kinachokwenda hewani kila ifikapo saa moja na nusu jioni kila siku kitakuwa na kipengere maalum kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. Samia.

Aidha wakati kipindi hicho kikiendelea kwenda hewani Viongozi mbalimbali wamepiga simu moja kwa moja studio na kutoa salamu zao za kumtakia kheri ya kuzaliwa Mhe.Rais Dkt.Samia.
Wakati kipindi icho kikiendele baadhi ya viongozi waliopiga simu katika kipindi hicho na kuzungumza moja kwa moja ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB bwana Abdulmajid Nsekela, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Christina Mndeme kwa wamesema Rais Dkt. Samia ni kiongozi shupavu na mwenye maono, tunamuombea kwa Mwenyeezi Mungu ampe uhai na hekima zaidi ili aendelee kuiongoza nchi yetu na kutoa wito pia kwa watanzania kuendelea kumshkuru Mungu kwa kutupatia Kiongozi msikivu Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Kwa upande wake Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa taarab nchini ambaye pia ni Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki Bi Khadija Omar Kopa ambae alikuwa ni mmoja ya mtoa burudani katika kipindi hicho aliimba wimbo mpya maalumu wenye mahadhi ya taarab.

"Rais Dkt. Samia mimi ni ndugu yangu namuombea mwenyeezi Mungu amzidishie nguvu na Ari ya kuliongoza taifa na kumzidishia umahiri wake katika kulitumikia taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Alisema Bi Khadija
Alisema Dkt. Samia ameingia katika kipindi kigumu cha uongozi lakini hivi sasa kila Mtanzania anakula mema ya nchi katika nyanja mbalimbali kama sanaa, michezo amekuza michezo ikiwamo soka ambako amekua akitoa hamasa ya goli la mama pamoja na mchezo wa masumbwi". Alisema Bi. Kopa.

Aidha Bi khadija Kopa aliongeza kuwa anamuombea kwa Mungu Rais Dkt.Samia aendelee kuiongoza nchi kwa amani na kusema mama ulipo tupo na huu ndiyo mwanzo wa ushindi.
Kwa upande wake msanii Barnaba Classic amesema anamshkuru sana Rais Dkt. Samia kutokana na hatua ambazo maekuwa akizichukua na kuonyesha alivyo na dhira ha dhati na upendo alionao kwa wasanii.

"Binafsi kama msanii ni moja ya mashahidi katika kipindi cha uongozi wake nimebahatika kuwa moja ya miongoni mwa wasanii ambao wanapata nafasi za kutoa burudani kwenye hafla mbaimbali za Serikali na Ikulu." Alisema Barnaba


No comments