Breaking News

PROF. MKUMBO: VYOMBO VYA HABARI VINA MCHANGO MKUBWA ELIMU DIRA YA TAIFA 2050

Dar es salaam - Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amevipongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kutoa taarifa juu ya Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 tangu ilipozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tarehe 11 Desemba 2024.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatatu Desemba 16, 2024.
Aidha amewaomba wanahabari kuripoti kwa weledi taarifa za Dira 2050 ili wananchi wapate taarifa kwa wakati na kwa usahihi.

Aidha ameanisha misingi mbalimbali iliyopo kwenye rasimu ya Dira 2050 kama umoja na mshikamano wa kitaifa , utu, uhuru na haki, demokrasia na misingi mingine.

Amekumbusha pia Shabaha 20 za Dira 2050 ambazo zinajumuisha uchumi ambao unatarajiwa kuchagizwa na uzalishaji wa ndani ya nchi, kuondoa umasikini na kuifanya Tanzania kinara wa uzalishaji wa chakula barani Afrika na kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa 10 wa chakula duniani.
 

No comments